Home Kimataifa City kufikisha alama 100? Swansea na Soton nani atashuka hii leo? tunaimaliza...

City kufikisha alama 100? Swansea na Soton nani atashuka hii leo? tunaimaliza Epl 2017/2018 hii leo

8536
0
SHARE

Southampton vs Manchester ​City, endapo leo City watashinda baasi itakuwa klabu ya kwanza kupata alama 100 katika historia ya EPL, lakini Southampton bado hawako salama na leo watacheza huku wakiangalia mchezo pia wa Swansea ila alama 1 tu itawaweka salama kubaki katika ligi kuu Uingereza. Japo tofauti ya mabao kati ya Soton na Swansea inatoa 60% kwa Swansea kushuka daraja.

Huddersfield vs Arsenal. Mchezo ambao umegubikwa na hisia zaidi siku ya leo, huu ndio mchezo wa mwisho kabisa kwa Arsene Wenger kama kocha wa Arsenal, mara ya mwisho Huddersfield kuifunga Arsenal ilikuwa 1971 na katika mecho 9 zilizopita hawajawahi kuifunga Gunners.

Liverpool vs Brighton. Katika michezo 26 iliyopita baina ya timu hizi mbili Brighton wamepata ushindi mara 4 tu, hii inawapa nafasi kupata walau alama moja hii leo ambayo itawahakikishia nafasi yao kushiriki Champions League msimu ujao.

Newcastle United vs Chelsea. Katika michezo minne iliyopita ya Newcastle katika uwanja wao wa nyumbani hawajawahi kufungwa na Chelsea huku wakifunga kuanzia bao mbili katika kila mchezo, hii leo Chelsea wanakwenda St James Park tena huku nafasi yao kucheza Champions League ikiwa mashakani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here