Home World Cup Road2Russia; Pele Amlilia Dani Alves

Road2Russia; Pele Amlilia Dani Alves

8066
0
SHARE

Na: DANIEL S.FUTE

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa Brazil Pele, amesikitishwa sana na taarifa kuhusu mchezaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa Brazil, Dani Alves kwamba hataweza kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Taarifa hii imetolewa baada ya mchezaji huyo kuumia kwenye goti katika mchezo wa Coupe de France akiitumikia klabu yake ya PSG. Shirikisho la Soka la Soka la Brazil (CBF) lilisisitiza kuwa mchezaji huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji kwenye sehemu aliyoumia mapema sana.

Kulingana na matatizo aliyo yapata beki huyu hata weza kwenda kuipeperusha bendera ya taifa lake mwezi ujao huko nchini Urusi. Hata hivyo kocha wa Brazil amesikitishwa pia na taarifa hiyo kutokana kwamba ana mkosa mtu sahihi ambae alikuwa kiongozi kwa wenzake.

“Ninasikitika sana kusikia hili,” mchezaji Pele mwenye mwenye umri wa miaka 77 aliandika katika ukurasa wake wa tweeter. “Wachezaji wanachukia kupata majeraha katika michezo ya mwisho ya ligi zao, wakitazamia kwenda kuziwakilisha timu zao za taifa lakini hali inakuwa tofauti baada ya kupatikana na majeraha, hasa katika michuano mikubwa kama hii ya Kombe la Dunia ni hisia mbaya sana.

“Hakuna kujiuliza tena, mahesabu yana tuonyesha ni kwamba atakuwa nje ya uwanja karibu miezi sita,” alisema Pele.

Habari za Alves mwenye umri wa miaka 35 ni pigo kwa mipango ya kocha Tite, maana mwezi Februari kocha huyu alithibitisha kwamba Alves ni mmoja ya wachezaji 15 bora wanao kiunda kikosi cha Brazil.

Wachezaji Danilo na Rafinha wana uwezekano mkubwa wa kuchukua nafasi ambayo ameicha Alves katika fainali za Kombe la Dunia, ambapo Brazil wanatarajia kuanza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Switzerland mnamo Juni 17.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here