Home World Cup Road2Russia: Je wajua? Pata vifurushi hapa

Road2Russia: Je wajua? Pata vifurushi hapa

7311
0
SHARE

Na Melkizedeck Mbise.

Mchezaji mkubwa kiumri kufunga goli katika historia ya kombe la Dunia ni mchezaji wa zamani wa Cameroon, Roger Milla ambapo alifunga akiwa na umri wa miaka 42 na siku 39, katika mechi dhidi ya Russia mwaka 1994. Michuano hii ilifanyikia Marekani ambapo bingwa alikuwa Brazil. Roger Milla anakumbukwa kwa style yake ya ushangiliaji ambapo alichezea pia vilabu kama – Montepellier, Monaco, Bastia na Saint Ettienne.

Mchezaji mzee zaidi kucheza katika historia ya kombe la Dunia ni Golikipa wa Colombia, Faryd Mondragon ambapo alikua na umri wa miaka 43 na siku 3, katika mechi ya Colombia vs Japan, ambapo Colombia ilishinda magoli 4 kwa 1. Michuano hii ikifanyikia nchini Brazil, pia Mondragon alianza soka mwaka 1990 ambapo amecheza ligi za nchi mbalimbali kama Colombia, Hispania, Ujerumani, Uturuki na Argentina. Ambapo alicheza mechi 51 katika timu ya taifa.

Tangu michuano ya kombe la Dunia mwaka 1966 zilizofanyika nchini Uingereza ambapo bingwa alikua Uingereza. timu ya taifa ya Brazil wamefunga magoli 36 nje ya boksi ambapo ni zaidi timu nyingine, zilizoshiriki michuano hii.

Katika historia ya michuano ya kombe la Dunia, jumla ya magoli 41 ni ya kujifunga, Hispania, Mexico na Bulgaria wamejifunga magoli 3 kila mmoja, hii ni idadi kubwa kwa timu moja.

Timu za taifa za Amerika Kusini ndo zenye uwiano mkubwa wa ushindi katika michuano ya kombe la Dunia, ambapo zina asilimia 48% ya ushindi katika jumla ya mechi zote walizoshiriki. Hii ni zaidi ya mabara mengine.

Je wajua?

Baada ya Juventus kushinda magoli 4 kwa 0 dhidi ya Ac Millan, kipa wa Juventus Gianluigi Buffon alitimiza clean sheet 300 akiwa na Juventus.

Baada ya Wilfried Zaha kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi 4 wa ligi kuu Uingereza, amekua mchezaji wa kwanza wa Crystal Palace kushinda tuzo hii toka mara ya mwisho Crystal walipotoa mchezaji mwingine 2004, Miaka 14 iliyopita. Zaha alishinda tuzo hiyo baada ya kucheza mechi 4, akafunga magoli 4 na assist/kutoa pasi 1 ya goli.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here