Home World Cup Road 2 Russia: Hii sio ya kukosa kabisa

Road 2 Russia: Hii sio ya kukosa kabisa

8708
0
SHARE
MAJINA YA UTANI KOMBE LA DUNIA 2018

Argentina – La Albiceleste (White and Sky Blues)

yaani mawingu meupe na ya buluu. Kikwetu tunasema mambo ni shwari.

Australia – The Socceroos

(kwa ufupi kabisa hakuna historia kamili au linganifu ya hili jina. Ni neno ambalo lilitumika kimazoea tu nchini humo. Asili ya neno hili linatokana na jina Kangaroos. Jina hili lilikuwa tayari limeshatumika na nchi nyingine na vilabu mbalimbali.

Mwandishi mmoja wa mjini SydneyTony Horsted huyu ndiye aliyetumia jina hili kwa mara ya kwanza kwenye gazeti mnamo mwaka 1967 wakati timu ya taifa ikiwa chini ya kocha Joe Vlasits, walipokwenda kucheza dhidi ya Vetnam ikiwa mwaka ule walikuwa wanatumia jina Emus ambapo ni ndege anayevutia zaidi kwa utalii nchini humo

Belgium – Les Diables Rouges (Red Devils)

Maana yake ni Mashetani wekundu kama ilivyo kwa Manchester United.

Asili ya Mashetani wekundi halina uhusiano na ushetani bali ni neo la kimichezo tu

Brazil – Selecao (The selection)

kutokana na brazil kuwa na vipaji vingi basi timu ya taifa hilo hutumia neno hilo kuwakilisha vipaji vingine ambavyo vimeachwa.

Wanaamini kuwa wale ni wateule tu lakini vipaji vingi vinakuwa wameachwa

Colombia – Los Cafeteros (The Coffee Growers)

hii ina maana ya wakulima wa kahawa. Colombia wanasifia sana kwa kilimo hicho

Costa Rica – Los Ticos (Spanish slang for Costa Rica natives)

hiyo ni lugha tu ya mtaani kumaanisha watu wa Costa Rica. Ni kama sisi tunavyotumia neno mbongo au mimi ni Mrombo

Croatia – Vatreni (The Blazers).

Hii inatokana na unifomu zao kuwa na madoadoa mengi. Blazers ni makoti yanayovaliwa na wanafunzi au wanamichezo huku yakiwa na rangi nyingingi.

Denmark – Danish Dynamite

(neno hili lina maana ya mlipuko)

Salah siku hizi anafahamika kama The Egyptian King au Farao wa Misri.

Egypt – The Pharaohs

Sisi tunawaita mafarao. Kuna watu wanadhani farao ni mtu mbaya. Hapana. Haipo hivyo. Farao ni cheo cha ufalme kule Misri. Ni kama sisi tu Rombo mfalme wetu huitwa Mangi. Sasa ukija huku mjini watu wanadhani Mangi ni muuza duka. Hapana. Mangi ni mfalme. Hawa jamaa wa Misri wanakuwaga na hujuma sana uwanjani. Juzi juzi wamevamia hadi kwenye mieleka kisa Mo Salah tu.

Wakiamua jambo lao labda aje Musa yule aliyewatumbukiza bahari ya Shamu ndiye anayeweza kuwatuliza.)

England – The Three Lions

Ukiacha wazaramo kwa kuongea sana wanaofuata ni waingereza. Wao wanajiita Simba watatu. Hii ni nembo inayotumika sana kimichezo nchini humo. Hata nembo ya ligi yao ni Simba. Tunaweza kusema Those are lions.

Manara akaona aibe haka kamsemo basi akawapachika wekundu wa msimbazi This Is Simba Brother)

France – Les Bleus (The Blues)

(Hili ni neo pia la kimichezo yaani wao wanajiita wa buluu kutokana na bendera yao na jezi zao.

Olivier Giroud France v Colombia
Imagehata sisis Hata sisi wabongo ni Les Blues

Germany – Die Mannschaft (The Team)

Ujue Ujerumani wanapenda sana vita vita. Wamekaa kama wakurya vile. wanajiita kikosi. Hawa jamaa walikuwa wanapenda sana vita. Ndio maana hata kwenye soka wana kikosi. Yaani wao wamekaa kijeshishi. Ispokuwa Ozil tu. Natania arsenal msije mkanipiga mawe.

Ukiachilia mbali vikosi vya jeshi la Hitler basi hata kwenye soka wao walikuwa na jeshi la Soka. Hata walokole nao wana majeshi. Jeshi la wakovu n.k

Iceland – Strakamir Okkar (Our Boys)

Ukienda Arusha utasikia machalii, mitaani watasema wahuni wangu, ukienda kwa wamasai wanaitwa Morani, Kenya utaambiwa mavijanaa.. Hi inamaanisha kuwa timu yao ya taifa ni kikundi cha Vijana wa kiume.

Iran – Shirane Pars (The Lions of Persia

Karne ya 5 baada ya Kristo wagiriki walikuwa na kiherehere sana. Waliitawala Iran ambapo walipabatiza Iran neno Median (Persia.

Kuna mwanaume mmoja alijukana na Cyrus the Great, huyo ndiye aliyeamua kuita neno hilo ambapo alitumia zaidi neno persa, kisha baadae wakabadili na kupaita Persika.

Kabla ya hapo Iran palijulikana kama Ardhi ya Waaryan au Iranshahr. Kiongozi wa wairan Reza Shah Palahvi mwaka 1935 aliuomba umoja wa mataifa kuondoa neno Persian na kuwaita Iran. Persia lilikuwa neno la kigiriki. Mwanae Reza ajulikanae kama Mohamed akautangazia umma kuwa majina yote mawili yaani Persia na Iran yatatumika kwa pamoja. Timu ya taifa ikaamua kutumia jina la awali na kujiita Simba wa Ardhini yaani Persia. Upo hapo?

Japan – Samurai Blue

Samurai si mnawajua wale washkaji wa kwenye movie wanakatana na mapanga?

Sijui kung fu na makaratee huko? Sasa hawa jamaa nao wameamua kujiita hivyo.

South Korea – Asian Tigers

maanake ni chui aina ya taiga ambaye ni chuo hatari zaid.

Mexico – El Tricolor

Bendera ya Mexico ina rangi 3, Nyekundu, Kijani na Nyeupe)wale wa mbagala wanajiitaje vile? Mbagala rangi tatu sio? Basi hawa nao wanatokea mbagalarangi tatu ya Amerika huko

Sema amebarikiwa wamebarikiwa sana warembo. Ni kama brazil tu. Walatino wanajiita wenyewe. Unamuona mtoto huyo? Kama hao hapo wapo Kondoa tu

Morocco – Atlas Lions

Morroco imetawalia na milima mingi. Hawa wanajiita simba wa Milima ya Atlas huko.

Yaani ndugu zangu wa Usangi wangejiita Simba aa Usangi au wale wa Usambara wangejiita Simba sa Usambara. Kitonga pia sijawasahau.

Nigeria's 2018 World Cup home kit

Nigeria – The Super Eagles

Zamani sana timu ya taifa ya Nigeria iliunganishwa na wazungu watalii wa England. Walipeleka kikosi kile nchini Uingereza.

Kipindi kile hawakuwa na uhuru. Walikuwa wanavaa Tisheti nyekundu. Walichezl michezo 9, Minne hawakuvaa viatu na walishinda yote lakini michezo mitano waliocheza na viatu walifungwa.

Washkaji walikuwa peku hawa lakini walikchafua sana huko ulaya

Kisha baadae walipata uhuru. Kwenye nembo yao wa taifa waliweka alama ya tai. Kisha bendera yao ilikuwa ya kijani. Wakaamua kujiita Green Eagles yaani tai wa kijani. Tai ni mnyama maarufu sana nchini humo. Baada ya kufungwa fainali na Cameroon wakaamua kubadili jina na kujiita Super Eagles. Yaani Tai hatari sana. Timu yao ya wanaaake inaitwa Super Falcon na timu ya vijana inaitwa flying eagles.

Panama – Marea Roja (The Red Tide)

hii ni aina ya kemikali inayopatikana fukwe za bahari hasa maeneo ya bandarini.

Kemikali hii husababishwa na msuguano wa vyuma vya meli na masalia ya vyuma baharini.

Nchini Panama hili limekuwa tatizo kubwa na limekuwa na madhara makubwa sana baharini maana husababisha vifo vya Samaki na huleta madhara kwa binadamu. Wao kwenye soka wanajiita ni ile kemikali.

Peru – Los Incas

mwaka 1433 alikuwepo jamaa mmoja ajulikanae kama Pachacuti Inca Yupanqui, yaani maanake Mtakatifu anayetikisha dunia.

Huyu alikuwa mtawala wa tisa kule Inca Cusco Peru. Wakati ule yaank karne ya 16 ilitokea milki iliyosemekana kubwa zaidi duniani. Iliitwa Inca. Milki ile ilitawala mataifa kama Argentine, Bolivia, Chile, Peru na Equador. Huyu jamaa alikuwa anaabudu jua mahali pajulinapo kama Qurikancha. Baadae utawala ule ulikuja kuvunjwa mwaka 1533 na mfalme wa kihispania Fransisco Pizzaro. Sasa Quenchuan ni jamii wa wahindi wekundu ambao walikuwa moja ya familia za kifamle zilizotawala Incas. Utamaduni ule upo mpaka sasa na hata asilimia kubwa ya waperu ni wahindi wekundu ambao bado wanaenzi milki ile. Timu yao ya taifa bado wanajienzi kaa kujiita hivyo.

Poland – Polskie Orly

The Polish Eagles) hawa nao wanajiita tai wa Poland

Portugal – Seleccao das Quinas (shields)

wareno ni watu wanaothubutu sana. Unamkumbuka Vasco Da Gama? Unaambiwa wareno wanaweza kufanya kitu kwa kujiamini. Jiulize yule Da Gama nani alimwambia azunguke na bahari hadi akafika afrika kusini? Kuna neno moja wareno hutumia “saudade” hawaogopi.

Timu yao ya taifa wanaitumia kama ngao. Wanachokiamini watakishikilia. Wanatuma ngao yao wakifanikiwa vyema wakishindwa pia vyema. Hao ndio wareno.

Russia – Sbornaya (Team)

wanajiita tu timu hawana mbwembwe kama raisi wao.

Warusi hawana mambo mengi. Ukisema timu inatosha.

Saudi Arabia finished as Group B runners-up in Asian qualifying

Image:

Saudi Arabia – Al Sogour Al Akhdar (The Green Falcons)

Kozi ni ndege mbua wadogo wa familia ya Falconidae. Wana mabawa membamba yaliyochongoka ambayo yanawapa upesi na uwezo wa kubadilisha mwelekeo upesi. Kozi tembere, ndege wepesi kabisa duniani, wanaweza kufika upesi wa kushuka wa zaida ya km 300 kwa saa. Tumeelewana? Hao wasaudia wanajiita huyo ndege. Huyo ndege alifahamika mwaka 1758 kipindi hicho nilikuwa bado mdogo sijaanza shule. Hivi hao ndege kwenu mnawaitaje? Au nawe kwenu Dar?

Senegal – Les Lions de la Teranga (The Lions of Teranga)

Germain Badang ambaye ni profesa alisema Teranga manake ni ukarimu.

Kwahiyo wasenegali wanajiita simba wakarimu. Ni hayo tu

Serbia – Orlovi (The Eagles)

hawa nao wanajiita tai

Spain – La Furia Roja (The Red Fury)

Kikosi chekundu. Ni kikosi cha wanajeshi hatari. Hatari sana. Hatari mnoo. Sasa sijui hawa ndo FFU wa kivita wa huko kwao au vipi?

Sweden – Blagult (The Blue and Yellows)

wanajiita wa buluu na manjano. Wanawakilisha bendera

Granit Xhaka has told Northern Ireland to stop complaining about the penalty decision at Windsor Park
Image:Granit Xhaka atakuwa mbeba msalaba mwekundu.

Switzerland – Rossocrociati (The Red Crusaders)

wanajiita wabeba msalaba mwekundu. Hii ni ishara iliyopo kwenye bendera yao

Tunisia – Les Aigles de Carthage (The Eagles of Carthage)

carthage ni utawala wa kitemi ulioanzsishwa mwaka 800 huko. Mjii huo ulikuja kukorofishana na warumi.

Mwaka 146 warumi wakafutilia mbali kale kamji kwa kukavamia na kuharibu kila kitu. Walageria bado wana uenzi mji huo.

Uruguay – Charruas (A warrior tribe in Uruguay)

kuna jamaa mmoja alijukana kama Jesuit Pedro Lozane, aliwalaano sana hawa charruas kwa kusababisha kifo cha mpelelezi wa kihispania ajulikane kama Juan Diaz mwaka 1515. Hawa charruas ni kama wale Rugaruga boys?

Yaani ni wale mamorani wa huko kwa akina Cavani zamani sana walikuwa wakipinga vikali uvamizi wa wakoloni. Wewe huoni hata miili ya akina Cavan Suarez?

Nadhani Cavan angekuwepo zamani hizo nae angekuwa Charruas.

Makala hii imeandaliwa na Privaldinho unaweza pia kunifollow (Instagram)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here