Home Kitaifa Kichuya, Kwasi, wapiga ‘mkwanja’ Singida

Kichuya, Kwasi, wapiga ‘mkwanja’ Singida

11871
0
SHARE

Kama kuna wachezaji wa Simba waliowashika mashabiki basi huwezi kuacha kuwataja Shiza Kichuya na Asante Kwasi ambao wanafanya vizuri na wamekuwa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Msimbazi.

Wawili hao leo wamepiga mkwanja kutoka kwa mashabiki waliokuwepo uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati Simba ikicheza na Singida United mechi ambayo imemalizika kwa Simba kushinda 1-0.

Wakati timu zikijiandaa kurudi uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili, Kwasi na Kichuya ambao walianzia kwenye benchi katika mchezo huo waliitwa na mashabiki na kuanza kupewa fedha.

Kitendo hicho ilibidi kizuiwe na jeshi la polisi kwa sababu kilianza kusababisha usumbufu na huenda kingesababisha vurugu kwa sababu kila shabiki alitaka kutoa kiasi cha pesa kwa wachezaji hao.

Kichuya na Kwasi watavaa medali ya ubingwa wa VPL kwa mara ya kwanza kwa sababu timu walizozitumikia kabla ha Simba hazikuwahi kushinda taji hilo. Kichuya alikuwa anacheza Mtibwa Sugar kabla ya kusajiliwa na Simba wakati Asante kwasi yeye amecheza Mbao na Lipuli kabla ya kuhamia Msimbazi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here