Home Dauda TV Kapombe afafanua style ya kushangilia, Niyonzima kafunguka

Kapombe afafanua style ya kushangilia, Niyonzima kafunguka

13460
0
SHARE

Shomari Kapombe ndiye aliifungia Simba goli pekee lililoamua matokeo ya mchezo dhidi ya Singida United.

Kapombe alishangilia kwa style iliyoashiria analea, baada ya mchezo alisema mkewake amejifungua mtoto wa kike ndiyo sababu iliyomfanya ashangilie kama anabembeleza mtoto.

“Zawadi ya goli hili kama mlivyoona nilipofunga nilishangilia kwa sababu nimepata mtoto wa kike, nashukuru Mungu kwa kunipa zawadi hii”-Shomari Kapombe.

Wakati huohuo kiungo wa Simba Haruna Niyonzima ambaye hajaonekana mara nyingi kwenye mechi za ligi amesema lengo la Simba ni kumaliza ligi bila kupoteza mchezo.

“Tumeshachukua ubingwa lakini malengo ya Simba ni kumaliza ligi bila kufungwa, hatuta poteza mchezo wowote licha kwamba kupoteza ni sehemu ya mchezo wa mpira”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here