Home Kimataifa Hamburg washuka daraja kwa mara ya kwanza katika miaka 55

Hamburg washuka daraja kwa mara ya kwanza katika miaka 55

9242
0
SHARE

Pamoja na Hamburg kupata ushindi wa mabao 2-1 lakini ushindi waliopata Wolfsburg wa mabao 4-1 dhidi ya Cologne umeifanya timu ya Humburg kushuka daraja ikiwa mara ya kwanza katika miaka 55.

Tangu mfumo mpya wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga uanzishwe mwaka 1963, klabu ya Hamburg imekuwa klabu pekee ambayo imewahi kushiriki misimu yote ya ligi ya Bundesliga.

Baada ya mashabiki wa Hamburg kufahamu timu yao imeshuka daraja walianza kurusha vitu vya mlipuko katikati ya uwanja na kuufanya mchezo huo kusimama kwa takribani dakika 10 kabla ya kuendelea tena.

Katika matokeo mengine ya kustaajabisha mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakiwa katika dimba lao la Allianz Arena wamekubali kipigo cha 4-1 kutoka kwa Vfb Stuttgart ambayo inashika nafasi ya 7 katika La Liga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here