Home Kimataifa Bale ndio mchezaji tajiri zaidi mwenye umri mdogo 2018

Bale ndio mchezaji tajiri zaidi mwenye umri mdogo 2018

9795
0
SHARE

Utafiti uliofanywa kuhusu wachezaji matajiri zaidi wenye umri chini ya miaka 30 unaonesha kwamba Gareth Bale ndiye mchezaji mwenye pesa zaidi katika orodha ya wachezaji umri chini ya miaka 30.

Jarida la Sunday Times limeonesha kwamba kwa sasa Gareth Bale anapokea kiasi cha £18.2m kwa mwaka, akiingiza pia £8m kutoka kwa wadhamini, na hii inamfanya kuingiza kiasi cha £78m kwa sasa.

Baada ya Gareth Bale anayefuatia kwenye orodha hiyo ni mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Argentina Sergio Aguero ambaye kwa sasa kwa mwaka anaingiza kiasi cha £48m.

Eden Hazard wa Chelsea anaingiza kiasi cha £32m kwa mwaka na anashika nafasi ya tatu huku nafasi ya nne ikienda kwa Mesut Ozil ambaye anaingiza £28m kwa mwaka na kisha Theo Walcott akiingiza £26m.

Paul Pogba wa Manchester United anaingiza £25m akiwa nafasi ya sita, akifuatiwa na Juan Mata anayeingiza £24m kwa mwaka huu tu, nafasi ya nane ni Willian wa Chelsea akiingiza £23m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here