Home Kitaifa Yanga baada ya Simba kutwaa ubingwa “tunakubali yaishe”

Yanga baada ya Simba kutwaa ubingwa “tunakubali yaishe”

12594
0
SHARE

Yanga ndio walikuwa mabingwa watetezi wa taji la VPL ambalo walikuwa nalo kwa misimu mitatu mfululizo lakini jana Alhamisi Mei 10, 2018 waliwa rasmi baada ya kufungwa Tanzania Prisons 2-0 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Baada ya kuutema ubingwa huo ambao umeenda kwa watani zao wa jadi Simba, uongozi wa Yanga kupitia Katibu Mkuu wake Charles Boniface Mkwasa amesema wamekubali matokeo na wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Siwezi kuwasemea wala kuwaambia chochote Simba kwa sababu siku zote adui yako mwombee njaa. Siwezi kusema lolote kwa sababu wenzetu wameanza vizuri, pesa wamezitumia vizuri sisi tumetereza tunakubali yaishe.”

“Haya ni mashindano ya mwaka mmoja mwaka mwingine yanaanza tena lakini naamini makosa yaliyofanyika Yanga mwaka huu hayawezi kujirudia tena mwaka ujao. Tunaamini mwakani tukiwa na afya njema tutarudi kwenye nafasi yetu.”

“Kuna msemo wa Kiswahili unasema ‘kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa’ kwa hiyo tunakubali kuna makosa ambayo yamefanyika, tumekuwa na wachezaji wenye majeruhi ya muda mrefu tangu tumeanza ligi hatukuwa na mwanzo mzuri tumekuwa tukipata ushindi finyu lakini ndio mwendo wa safari.

“Tunakubali matokeo, tunajipanga kwa ajili ya mwakani.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here