Home Kitaifa “Sijawahi kuwa na furaha ya kiwango hiki, labda nilipooa”-Manara

“Sijawahi kuwa na furaha ya kiwango hiki, labda nilipooa”-Manara

10719
0
SHARE

Baada ya Yanga kufungwa 2-0 na Tanzania Prisons, moja kwa moja ubingwa wa VPL 2017/18 umeenda Msimbazi. Haji Manara anakwambia furaha aliyonayo haipimiki inaweza kuvunja mzani!!

“Sijawahi kuwa na furaha ya kiwango hiki, mara ya mwisho kuwa na furaha kama hii labda nilipooa na nilipopata watoto, sijawahi nansikumbuki.”

“Tumechukua ubingwa bila kufungwa sasa kipaumbele ni kumaliza ligi bila kufungwa.”

“Huu ni ubingwa wa mashabiki wa mpira hususan wa Simba, ubingwa wa jasho na damu, ubingwa tulioupigania, ubingwa tulioupata kwa haki bila figisu bila mtu kulalamika na imekuwa heri wametupa ubingwa wale waliokuwa wanadhani Mungu ni wao peke yao.”

“Tunafanya mpango maalum wa sherehe kubwa ambayo hakuna klabu yoyote ya mpira imewahi kufanya Tanzania baada ya kuwa mabingwa kwa sababu ubingwa huu ni halali na umesubiriwa kwa hamu.”

Manara anasema ubingwa umemkuta chumbani wala alikuwa hakuangalia mechi ya Tanzania Prisons vs Yanga ambayo ndio imewapa ubingwa VPL 2017/18.

“Ubingwa umenikuta chumbani Morena Hotel Dodoma, nilizima simu baadae nikawasha ili kupata matokeo kwa sababu hata sikuangalia mpira, baada ya kuwasha simu nikagundua tumekuwa mabingwa.”

Ubingwa wa VPL umebadilisha jina la Manara ametangaza rasmi na anaweza akamchapa mtu makofi endapo atakosea jina lake.

“Mimi ni msemaji wa mabingwa wa nchi ielewwke hivyo, mtu atakaeniita Haji Sunday Manara msemaji wa Simba nampiga vibao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here