Home Kitaifa Manara kapeleka ubingwa nyumbani kwake

Manara kapeleka ubingwa nyumbani kwake

13828
0
SHARE

Haji Manara ameupeleka ubingwa wa VPL nyumbani kwake kwa kuu-dedicate ubingwa huo kwa familia yake.

Manara amesema familia yake ilikuwa na uvumilivu wa kiwango cha juu katika kipindi chote ambacho Simba ilishindwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

“Ubingwa huu nau-dedicate kwa familia yangu maana nimetukanwa, nimefedheheshwa na kudhalilishwa kwa miaka minne sio kama sisomi wala sioni. Simba ikifungwa natukanwa mimi, familia yangu ilikuwa na uvumilivu wa kiwango cha juu sana.”

“Wanasikia, wanaona, wakati mwingine hata nikitoka nao out napata mfedheheko hasa siku Simba ikifungwa au kutoka sare lakini wao walikuwa wavumilivu sana.”

“Wakati mwingine unatamani kuiacha Simba kutokana na hasira za huko nje lakini siku zote wamekuwa na mimi. Mama yangu amekuwa akiniunga mkono sana najua atakuwa na furaha sana.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here