Home Kitaifa Manara aishukuru Tanzania Prisons kwa ubingwa

Manara aishukuru Tanzania Prisons kwa ubingwa

9333
0
SHARE

Simba imetwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzanianbara 2017/18 wakiwa hotelini baada ya Yanga ambao walikuwa wapinzani wao wakubwa katika mbio za ubingwa kufungwa 2-0 na Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine Mbeya.

Ubingwa huo ulikuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu umekuja wakati Simba ikiwa hotelini Dodoma wakielekea Singida kwenye mchezo wao dhidi ya Singida United ambao walitaka kutangaza ubingwa katika mchezo huo endapo wangepata matokeo lakini shughuli imerahisishwa na Prisons.

Manara amewashukuru Tanzania Prisons kwa kuwarahisishia kazi na kusema watu wa Mbeya ni ndugu zake kwa sababu aliwahi kusoma huko.

“Kwanza mimi sekondari nilisoma Chimala-Mbeya, jina langu kwa upande wa babu aliyenizalia shangazi ni mnyakyusa, zamani walikuwa wananiita Haji Mwamanara kwa hiyo nawashuru sana wanyakyusa wenzangu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here