Home Kitaifa Baada ya ubingwa Rage aibuka ‘kuwazodoa’ Yanga

Baada ya ubingwa Rage aibuka ‘kuwazodoa’ Yanga

10247
0
SHARE

Kweli kutesa ni kwa zamu au unaweza kuita ‘kulia kupokezana’, baada tu ya mnyama kutangaza ubingwa wa VPL msimu huu, aliyewahi kuwa mwekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amewapiga kijembe Yanga kwa kuwaambia waliona wapi Simba anafukuzwa kwa bakora?

Simba iliongoza ligi kwa muda mrefu lakini watani wao wa jadi Yanga walikuwa na msemo wao ‘tunamfukuza mwizi kimyakimya’ na kuna wakati walizifikia pointi za Simba tofauti ikawa ni wastani wa magoli jambo ambalo lilianza kuzua hofu kwa baadhi ya mashabiki wakiamini huenda Yanga ikawapiga bao.

“Nilikuwa nina imani kubwa Simba itapata ubingwa kabla ya kucheza na Singida United na sababu kubwa ni majina yale ya kifedhuli tuliyokuwa tunaitwa “tunamfukuza mwizi kwa bakora.”

“Uliona wapi Simba anafukuzwa kwa bakora? Simba anafukuzwa kwa SMG bwana, sasa watani zangu wa Yanga waendelee na kazi mpya walioinza ya kuvua kambale pale kwenye shamba lao la samaki.”

“Sasa mwakani Yanga ndege watakuwa wanaisikia tu, ligi watakayokuwa wanacheza ni ya kwenye viwanja vya Maji Matitu, Tandale na Manzese.”

Rage amesema mshikamano ndani ya Simba ndio siri pekee ya timu yao kufanya vizuri msimu huu na kutwaa taji la VPL.

“Wanachama, wapenzi, mashabiki, wachezaji na viongozi waliweka pembeni tofauti zao wakaona kwamba kwakua safari hii wamesajili timu nzuri wawekeze kwenye kupata ushindi halafu mambo yetu yatafuata baadae lakini kwanza ni kutafuta ubingwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here