Home Kimataifa Yaliyojiri katika Ulimwengu wa Soka baada ya mechi za jana.

Yaliyojiri katika Ulimwengu wa Soka baada ya mechi za jana.

9165
0
SHARE

Klabu ya Manchester City baada ya ushindi wa magoli 3 kwa 1 dhidi ya Brighton & Hove Albion, City wameweka rekodi ya hizi;
-Timu ya kwanza kushinda mechi nyingi ambapo wameshinda mechi 31, wamevunja rekodi ya Chelsea msimu ulioisha 2016/17, ambapo walishinda mechi 30.

-Manchester City imekua timu ya kwanza ligi kuu Uingereza kufunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja ambapo mpaka sasa wamefunga magoli 105 ambapo wamevunja rekodi ya Chelsea msimu 2009/10 ambapo walifunga jumla ya magoli 103.

-City inakua timu iliyokusanya alama nyingi ndani ya msimu mmoja ambapo mpaka sasa wana alama 97, ambapo Chelsea ndo walikua wanashikilia rekodi hii msimu wa 2004-05 wakati walipokusanya alama/points 95.

Pia ikumbukwe Manchester City walishaweka rekodi nyingine ya kuwa timu ya kwanza ligi kuu Uingereza kuwa na wachezaji wanne wenye pasi za magoli zaidi ya 10. Kevin De Bruyne na Leroy Sane wana pasi 15, Raheem Stearling na David Silva wana pasi 11.

Baada ya Arsenal kufungwa na Leicester kwa magoli 3 kwa 1 jana, Arsenal imekua ni timu pekee katika ligi nne za Uingereza (yaani ligi kuu -Barclays premier league-, championship, daraja la kwanza na la pili) pasipo kushinda mechi yoyote ya ugenini tangu mwaka 2018 uanze, ikiwa wamecheza jumla ya mechi 7 hadi hivi sasa.

Baada ya Juventus kushinda kombe la Coppa Italia jana katika ushindi wa magoli 4 kwa 0 dhidi ya Ac Milan katika dimba la Estadio Olympico, kocha wa Juventus Massimiliano Allegri anakua kocha wa kwanza katika historia kutwaa taji hilo mara 4 mfululizo, ambapo ametwaa msimu wa 2014/15, 2015/16, 2016/17, 2017/18. pia Juventus inakua timu iliyotwaa ubingwa huo mara nyingi wakiwa wametwaa mara 12, wakifatiwa na Roma mara 9, Inter Milan mara 7, Fiorentina mara 6, Ac Milan mara 5, SSC Napoli mara 5 na Torino mara 5.

.

Je wajua?

Klabu ya Roma katika michuano ya Ligi ya Mabingwa walipata faida ya zaidi ya Euro Millioni 100?
-Euro Milioni 95 Ligi ya mabingwa Ulaya.
-Euro Million 16.5 Wadhamini
-Euro Milioni 5.5, tiketi zilizouzwa katika mechi ya Liverpool.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here