Home Kitaifa Simba bingwa VPL 2017/18

Simba bingwa VPL 2017/18

11231
0
SHARE

Kipigo cha 2-0 ilichochezea Yanga kutoka kwa Tanzania Prisons, kimeivua rasmi ubingwa wa VPL ambao unakwenda mitaa ya Msimbazi kwa Simba ambayo hata ikipoteza mechi zake zote (3) bado hakuna timu ambayo itaweza kuifikia.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 65 baada ya kucheza mechi 27, imebakiza mechi tatu kabla ya msimu wa ligi haujaisha. Yanga ambayo ilikuwa bingwa mtetezi inaendelea kubaki na pointi zake 48 baada ya kuheza mechi 25 na kubakiza mihezo mitano (5).

Endapo Yanga itashinda michezo yote mitano iliyosalia itafikisha pointi 63, ambazo ni pointi mbili nyuma ya Simba.

Ubingwa wa VPL utaipa Simba kombe, fedha taslimu lakini pia wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kombe la vilabu bingwa Afrika msimu ujao 2018/19 mashindano ambayo waliheza mara ya mwisho msimu wa 2012/13.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here