Home Kimataifa Samatta kaamka Ubelgiji

Samatta kaamka Ubelgiji

11170
0
SHARE

Hatimaye Mbwana Samatta ametumbukia nyavuni kwa mara ya kwanza kuifungia klabu yake katika mchezo wa ligi tangu kuanza kwa mwaka 2018.

Samatta ambaye alikuwa anakabiliwa na majeraha ya muda mrefu kabla ya kurejea uwanjani aliifungia klabu yake goli lake la mwisho mwezi Oktoba 2017 katika mchezo ambao KRC Genk ilishinda 2-0 dhidi ya KAA Gent.

Akiingia dakika ya 54 kuchukua nafasi ya mshambukiaji Nikolaos Karelis huku timu ikiwa nyuma kwa bao 1-0 Samatta alisawazisha goli hilo dakika ya 66 kuinusuru KRC Genk na kichapo kutoka KAA Gent.

Mchezo huo ulikuwa ni wa play off kwa ajili ya kupambania nafasi ya kuheza michuano ya UEFA Europa Liague na UEFA Champions League msimu ujao.

Genk ina pointi 32 ikiwa katika nafasi ya sita (6)  huku ikiwa imesalia michezo miwili, ili ijihakikishie kucheza mashindano ya Ulaya msimu ujao ni lazima imalize katika nafasi nne za juu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here