Home Kitaifa yupi ndiye mchezaji bora chipukizi VPL

yupi ndiye mchezaji bora chipukizi VPL

11622
0
SHARE

Baadhi ya wachezaji chipukizi wanaofanya vizuri msimu wa 2018

ADAM SALAMBA MIAKA 21-LIPULI FC
Alizaliwa tarehe 25-11-1997 kule Kakola Shinyanga. Ni mtoto wa pili katika Familia ya mzee Salamba. Yeye ni mshambuliaji wa kati yaani namba 9. Ni mchezaji bora wa Mwezi Machi. Ameonesha kiwango kikubwa kabisa katika klabu ya Stand United kabla hajaamia Lipuli
MARCEL KAHEZA MIAKA 24-MAJIMAJI
Kwa ligi ya Tanzania mchezaji wa miaka 24 ni mdogo. Ni moja kati ya wachezaji wazuri sana walioibuka na kuonesha kiwango kikubwa sana msimu. Ana umri mdogo. Ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa April kwa kuonesha kiwango kikubwa sana. Mwezi wa 4 alifunga mabao 7.
HABIB KYOMBO MIAKA 19-MBAO FC
Habibu Kyombo alizadiwa jezi na Simon Msuva kwa kiwango bora alichoonesha. Aliweka pia rekodi ya kucheza michezo mingi licha ya kuwa na umri mdogo. Habib Kyombo pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi desemba. Kufikia mwezi wa 4 aliifungia Mbao mabao 9.
SHABAN IDD MIAKA 19-AZAM FC
Alizaliwa kule Mtwara tar 20 Julai 1998. Bao lake la juzi dhidi ya Mbao ni bao lake la 3 dhidi ya Klabu hiyo ya Mbao. Mwaka 2016 alionesha kiwango kikubwa na kuwaacha walio wengi mdomo wazi. Bado kipaji chake kinazidi kukua siku hadi siku. Mwl Stewart hall ndiye aliyeona kiwango cha mmakonde huyu na kumpa nafasi ili aweze kuonesha makeke yake?
YUSUF MHILU MIAKA 23- YANGA
Ni mmoja wa makinda waliokuja kuokoa jahazi la Yanga lililokumbwa na majeruhi wengi. Amekuwa msaada mkubwa kwa timu na kila mara alipoingia uwanjani. ni mchezaji mwenye shauku ya kufanikiwa na kila mara aliopewa nafasi basi hakufanya makosa.
YUSUPH MLIPILI MIAKA 23-SIMBA
Alianzia maisha yake pale Toto Afrika kabla hajatua Simba. Joseph omog hakumwamini sana lakini Mwl Msaidizi Msoud alionekana kumwamini. Hata kocha mzungu Piere nae amemwani kiasi cha kumweka Cortey Benchi. Ni moja kati ya mabeki wanaojituma sana msimu huu.
ALLY ALLY MIAKA 24- STAND UNITED
Huyu kule shinyanga wanamuita Ally Mwarabu. Ana umbo dogo lakini ni mmoja kati ya mabeki visiki kabisa. Ameonesha uwezo mkubwa. Mzaliwa huyu wa Gulioni kule Zanzibar nae ni mmoja kati ya makinda ambao huenda dirisha la usajili akawindwa na vilabu vikubwa. Ni beki mzuri na anayejituma
RAMADHAN KABWILI MIAKA 17-YANGA
Bila shaka huyu ni moja ya lulu za hapo baade. Kama ataendelea kujituma hasa na kuwekeza akili yake zaidi kwenye soka basi hawa ndiyo akina Ivo Mapunda na Juma kaseja wa baadae. Kocha mkuu Lwandamila ambaye kwa sasa anaifundisha Zesco ya Zambia alimwamini sana bwana mdogo huyu hasa katika michuano ya kimataifa. Hakika anahitaji pongezi kwa kiwango chake.

Hii ni orodha ya wachezaji wachanga ambao wameonesha kiwango bora kabisa msimu huu. Unaweza kupiga kura hapo kwamba ni mchezaji gani anafaa kutwaa tuzo ya mchezaji bora bora chipukizi mwaka huu. Pia unaweza kutaja jina la mchezaji mwingine yeyote. Hii imeandaliwa na shadaka sports Management. Kama una mchango wowote toa maoni yako pia

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here