Home Kimataifa Manchester United yatajwa kuwa brand ghali zaidi katika vilabu vya soka duniani

Manchester United yatajwa kuwa brand ghali zaidi katika vilabu vya soka duniani

14398
0
SHARE

Utafiti uliofanywa na kampuni ya Brand Finance inayohusiana na brands/chapa katika soka uliofanyika mwaka 2018 unaonesha kwamba klabu ya Manchester Unites ndio brand ghali zaidi kwa sasa.

Utafiti unaonesha thamani ya klabu hiyo ni kiasi cha £1,325 millions na japokuwa hawajachukua kikombe chochote kikubwa inawafanya kuwa juu ya vilabu vyote duniani ikiwemo Real Madrid na Liverpool ambao wako nusu fainali ya Champions League.

Real Madrid wako nafasi ya pili ambapo thamani ya klabu hiyo katika chapa ni £1,127millions, huku klabu ya Barcelona ikishika nafasi ya tatu katika orodha hiyo ambako Barca wana thamani ya £1,082m na kisha Bayern Munich wakiwa na thamani ya £1,007m.

Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza ambao ni wapinzani wakubwa wa United, Manchester City wako katika nafasi ya 5 ambapo thamani ya brand ya klabu hiyo inayomikiwa na matajiri wa Quatar ni £953m.

Baada ya City kuna vilabu vya Uingereza vitatu vimeongozana ambapo kuna Liverpool(£862m), wapo Chelsea (£856m), kisha Arsenal (£776m), baada ya hapo wanafuata vinara wa Ufaransa PSG(£654m) na wanamalizia Tottenham Hotspur katika nafasi ya 10(£547m).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here