Home Kimataifa Hivi unajua kwanini City kabeba EPL? hizi hapa nguzo zao 5 zilizowapa...

Hivi unajua kwanini City kabeba EPL? hizi hapa nguzo zao 5 zilizowapa ndoo

7987
0
SHARE

Tayari Manchester City wamechukua ubingwa wa EPL, na japo ligi haijaisha lakini City wameshaweka rekodi kuwa timu ya kwanza EPL kuchukua ubingwa wakiwa na alama nyingi zaidi 97, Gurdiola anaonekana kuijenga City kwa namna ambayo kila mmoja anaona kweli huyu ni tactic master lakini sababu hizi 5 zimechangia kwa zaidi ya 85% City wakawa mabingwa msimu huu.

1.Mawinga halisi. Hivi uliiona Baraca ya Pep? Alikuwa akitumia mastriker ambao walikuwa wakitokea pembeni, David Villa, Thiery Henry na Pedro Rodriguez walikuwa sehemu ya mpango huu. Alipofika Bayern akatumia mawinga ambao walikuwa wanacheza kuwa kuingia ndani zaid kwenye lango la wapinzani Franck Ribery na Arjen Roben wakampa matokeo.

Lakini hapa Man City msimu huu Pep amekuja na mawinga halisi, Leroy Sane ni 11 halisi kwani anachezea mguu wa kushoto na Raheem Sterling ni 7 halisi akitumia mguu wa kulia, uchezaji wa nyota hawa wawili kwenye flanks zao ulikuwa ukileta matatizo makubwa sana kwa mabeki wa pembeni wa upinzani na wataalamu wa mambo wanasema uchezeshaji huu wa mawinga ulionekana mara ya mwisho wakati Blackburn Rovers wakibeba EPL 1994/1995.

2.Kuuficha mpira. Ni makocha wachache sana waliofanikiwa kuuona mpira mbele ya Gurdiola, Pep msimu huu alielekeza nguvu zake katika kuuficha mpira na rekodi zinaonesha kwamba wakati Leicester akibeba ndoo alimiliki mpira kwa 44% tu msimu mzima lakini hadi sasa Man City wamemiliki mpira kwa 66.4% na wanaowafuatia ni Tottenham na Arsenal ambao wamemiliki mpira kwa 58%, Acha hilo lakini pia City wamekamilisha pasi msimu huu kwa 84% ikiwa ni rekodi kubwa ya pasi timilifu kwa msimu.

 3.KDB na Silva. Hivi unaachaje kuizungumzia City bila De Bruyne, unazungumziaje ubunifu wa City bila David Silva?. Uhuru ambao Pep amewapa De Bruyne na Silva katika eneo la kati la uwanja umeifanya mipira kuwa rahisi sana kwenda kwa winga za pembeni na hii iliwafanya City mara nyingi kuonekana kana timu yenye chemistry kubwa kati ya kiungo ushambuliaji na eneo la washambuliaji na hii ikawa janga la wapinzani msimu huu.

4.Kipa kama kiungo. Kati ya mambo ambayo Pep Gurdiola anajivunia sana ni Ederson, pamoja na kuwa golikipa lakini Ederson anaonekana kuwa chanzo cha mashambulizi ya City, katika fainali ya Carabao Cup mpira aliopiga ulikuwa chanzo cha bao la Sergio Aguero. Ederson amekuwa anapiga mipira mirefu na mara nyingi inaangukia mahala sahihi kwenye zone ya ushambuliaji ya City na kuwa rahisi kwao kusogea mbele.

5.Pasi za ziada. Msimu huu Sterling amekuwa on gire zaidi kutokana na pasi za ziada ambazo City wanapiga, Sterling amekuwa akifunga mabao ya wazi na tap-ins kutokana na aina hii ya mchezo. City wanachofanya ni kupiga pasi nyingi sana na hii imekuwa ikiwasaidia kutengeneza mashambulizi haswa wanapokuwa katika eneo la 3 la wapinzani, hii pia imefanya assist kuwa rahisi kwa kila nyota wa City na ndio maana hadi sasa De Bruyne ana assist 15, Sane ana 12 huku Silva akiwa na 11.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here