Home Kimataifa Japo ligi haijaisha lakini Epl msimu ujao inasisimua zaidi kuliko hii

Japo ligi haijaisha lakini Epl msimu ujao inasisimua zaidi kuliko hii

9920
0
SHARE

Baada ya leo inakuwa bado mchezo mmoja mmoja ili ligi ya EPL iweze kumalizika, mengi yametokea na Man City kabeba ubingwa huku nne bora ikionekana inaweza kubaki kama ilivyo, lakini tayari naiona EPL ya msimu ujao ikiwa ya kusisimua kabla hata hii haijaisha?

Mo Salah, Salah ni one season wonder? Hili limekuwa swali tunalojiuliza wengi wetu, kuna watu wameshaanza kumfananisha Salah na Lionel Messi japo kiuhalisia Salah hajafika alipo Messi, kumkuta Messi inabidi afanye hiki anachokifanya kwa misimu angalau mitatu, sasa swali je msimu ujao wa ligi Salah atafanya hiki afanyacho sasa?

Jose Mourinho. Tunasubiri kuona nini Mou atafanya, amekosa ubinwa wa EPL kwa mara ya pili mfululizo katika timu moja na hii ikiwa mara yake ya kwanza kucheza misimu miwili na kutoka kapa, United walitumia pesa kubwa dirisha lililopita la usajili, Mourinho atatoa tena pesa nyingi ya usajili kurudisha heshima? Au atakomaa na kikosi kilichopo aiwinde Man City tena?

Pep Gurdiola. Kikosi cha msimu huu cha Man City kinatajwa kama kati ya vikosi bora zaidi kuwahi kubeba EPL, alama 97+ walizochukulia ubingwa pamoja na michezo waliyoshinda inatosha kuonesha ubora wa City, lakini tunasubiri kuona namna ambavyo Pep Gurdiola anaweza akaendeleza timu hii.

Jurgen Klopp. Ukitaja timu bora kwa sasa barani Ulaya kutokana na michuano ya Champions League baasi Liverpool ipo, moto waliouwasha hivi karibuni unaogopesha kila mtu, kwa namna ambavyo wanacheza inaonekana timu ambayo inakuwa na asilimia kubwa kushinda kila mechi, inaweza kuwa msimu ujao wakawa na changamoto kubwa sana katika mbio za ubingwa.

Arsenal. Hivi umeshawahi kuizungumzia Arsenal bila Wenger, umeshawahi kukaa miezi miwili bila kuona bango la “Wenger Out”. Sasa walichokisubiria Arsenal kwa muda mrefu kimetokea, Arsenal watakuwa bila mzee Wenger tangu kabla ya mwaka 1996. Hii inafanya kila mtu asubiri kuona ni kweli babu hakuwa mtu sahihi Arsenal na nini kinaletwa na kocha ajaye.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here