Home Kitaifa Yanga yaomba kutazamwa kwa huruma “wawe na huruma tunapambana na hali zetu”

Yanga yaomba kutazamwa kwa huruma “wawe na huruma tunapambana na hali zetu”

11566
0
SHARE

Leo Jumatano Mei 9, 2018 mwenyekiti wa matawi ya Yanga Tanzania Bakili Makele ametoa malalamiko kwa TFF na kuiomba iwaangalie kwa namna ya kipekee hususan katika kipindi hiki ambacho klabu ina matatizo ya kiuchumi.

Yanga imeilalamikia TFF kwa kutotoa mwakilishi ambaye angeongozana na timu kwenda Algeria ambako Yanga ilicheza mechi ya makundi kombe la shirikisho Afrika na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa 4-0 na wenyeji wao USM Alger.

TFF inalalamikiwa kuitoza Yanga zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufidia mambo mbalimbali ikiwemo kodi, gharama za uwanja na mambo mengine katika mchezo wao dhidi ya TP Mazembe ambapo mashabiki waliingia bure katika mchezo huo.

Yanga wameiambia TFF kama inawadai basi fedha hizo wakate katika milioni 200 waliyowatoza katika mchezo dhidi ya TP Mazembe.

Yanga wanadai TFF imezuia pesa zao zaidi ya shilingi milioni 23 kutoka kwa mdhamini mkuu wa ligi kuu kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom.

Malalamiko ya Yanga yamegusa hadi mashindano ya kombe la shirikisho Afrika ambayo wanashiriki sasa kwamba kuna vifaa ambavyo vimetumwa na Caf kupitia TFF lakini bado havijawafikia.

Makele ameiomba TFF kuiangalia Yanga kwa jicho la huruma kama mlezi, “wawe na huruma hali yetu mbaya kiuchumi tunapambana na hali zetu tunaiendesha klabu katika mazingira magumu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here