Home Uncategorized Taarifa mbalimbali za Majuu

Taarifa mbalimbali za Majuu

9932
0
SHARE

IMEBAKI miezi miwili kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia ambayo inatarajia kufanyika nchini Urusi.

Kama ilivyo kawaida michuano hii ni michuano ambayo inabeba hisia kwa kila mtu, kuanzia mashabiki,wachezaji,makocha hata waamuzi.

Alhamisi ya jana FIFA ilithibitisha orodha ya waamuzi ambao watakuwa washiriki katika fainali hizo za Kombe la Dunia huko Urusi.

Waamuzi ambao wamechaguliwa na FIFA ni waamuzi 36 pamoja na wasaidizi 63, katika michezo yote ambayo itachezwa katika viwanja tofauti tofauti nchini Urusi.

Katika waamuzi hao, Ligi kuu ya Marekani ‘MLS’ wameweza kutoa waamuzi wawili, tofauti na Ligi kuu ya England ambapo msimu huu wameshindwa kutoa waamuzi ambao watachezesha michezo hiyo ya Kombe la Dunia.

Waamuzi ambao wamechaguliwa na FIFA katika Fainali hizo ni Mark Geiger na Jair Marrufo.

*Moutinho Akubali Mkataba Mpya*

MCHEZAJI wa As Monaco Joao Moutinho, amekubali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu yake hiyo.

Moutinho ameweza kuongeza mkataba wa miaka miwili, ambao utambakiza klabuni hapo mpaka kufikia mwaka 2020.

Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye miaka 31, amekuwa mchezaji wa Monaco tangu mwaka 2013 baada ya kutoka Fc Porto.

“Ninafurahi sana kuendelea kuwa mchezaji wa Monaco, baada ya kupatiwa mkataba mpya ambao utakuwa muhimu kwangu pamoja na klabu yangu,” alisema Moutinho.

*Ben Arfa Kuondoka PSG*

HATEM Ben Arfa ametangaza rasmi kupitia mtandao wake wa Instagram, kwamba anatarajia kuondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu.

Ben Arfa ambaye hajajumuishwa katika kikosi cha PSG tangu Aprili 2017, ambapo klabu yake iliibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Avranches.

Mwanasheria wa mchezaji huyo amewashtaki PSG baada ya kukiuka mkataba wa Mfaransa huyo, na amesema kwamba Ben Arfa hawezi kuendelea na klabu hiyo ifikapo mwisho wa msimu huu.

Zimeandaliwa na: *Daniel S.Fute*

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here