Home Kitaifa Ridhiwani anautaka uenyekiti Yanga?

Ridhiwani anautaka uenyekiti Yanga?

10428
0
SHARE

Baadhi ya magazeti ya leo Jumatano Mei 9, 2018 yameripoti kwamba, Ridhiwani Kikwete anahusishwa kuwania nafasi ya uenyekiti ndani ya klabu Yanga nafasi ambayo kwa sasa ipo wazi tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti Bw. Yusuf Manji.

Ridhiwani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze amesema hana lengo la kutaka uongozi ndani ya klabu hiyo kwa sababu yeye ni shabiki na hana kadi ya uanachama wa Yanga hivyo hana sifa za kugombea uongozi.

“Sina lengo lolote la kutaka uongozi ndani ya Yanga labda wanachama wenyewe ndio wanatengeneza maneno hayo lakini mimi binafsi hakuna sehemu nimewahi kutamka.”

“Hata wale waliowahi kunifuata kuniuliza au kuniomba ushauri kuhusu mambo mazuri ambayo yanaweza kufanyika, sijawahi kutaja kwamba nataka kugombea uongozi kwa sababu sioni kama naweza kuiongoza Yanga kwa sasa kutokana na kazi zangu na mambo ninayokimbizana nayo kwa wakati huu.”

“Mimi naweza kuwa shabiki maarufu wa Yanga lakini sio mwanachama kwa sababu sina kadi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here