Home Uncategorized Huddersfield wabaki ligi kuu huku Gurdiola akiivunja rekodi ya Mourinho

Huddersfield wabaki ligi kuu huku Gurdiola akiivunja rekodi ya Mourinho

9260
0
SHARE

Alama moja katika uwanja wa Stamford Bridge umeihakikishia klabu ya Huddersfield kuwepo katika ligi kuu nchini Uingereza katika msimu ujao, matokeo ya leo yanawafanya kufikisha alama 37 katika msimamo wa ligi alama ambazo zinawahakikishia uwepo katika ligi kuu.

Habari nyingine kubwa katika mchezo wa leo ni namna ambavyo kocha wa Chelsea Antonio Conte alikipanga kikosi chake akimuacha Eden Hazard nje pamoja na Olivier Giroud na alama moja waliyoipata hii leo inawaweka katika hatihati kushiriki Champions League msimu ujao.

Suluhu ya leo ya Huddersfield inamaanisha kwamba timu zote zilizopanda daraja msimu huu zinabaki ligi kuu na hii ikiwa ni mara ya tatu katika historia ya Epl kwa jambo kama hili kutokea ambapo ilishatokea msimu wa 2001/2002(Blackburn, Fulham na Bolton) na ikatokea pia 2011/2012(Swansea, Norwich na Qpr).

Kwingineko mabao mawili ya Riyad Mahrez na moja la Jamie Vardy yalitosha kuiua Arsenal bao 3 kwa 1, ambapo matokeo haya yanawafanya Arsenal kuwa timu ambayo inaongoza kwa matokeo mabovu ugenini kuliko timu yeyote katika ligi kuu 5 kubwa barani Ulaya kwa mwaka 2018.

Manchester City waliipiga Brighton & Hove Albion mabao 3 na hii kuwafanya City kushinda michezo 31 katika msimu huu wakiifikia rekodi ya Tottenham waliyoiweka 1960/1961 ya kushinda idadi ya michezo kama hiyo katika ligi, lakini pia Gurdiola anakuwa ameivunja rekodi ya Jose Mourinho ya kumaliza ligi akiwa na alama nyingi ambapo Pep amefikisha 97, huku Mou alifikisha 95 msimu wa 2004/2005.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here