Home Kitaifa Yanga yarudisha nembo ya mdhamini

Yanga yarudisha nembo ya mdhamini

12682
0
SHARE

Uongozi wa Yanga umesema tayari wamefanikiwa kumaliza tatizo lililosababisha timu yao kushindwa kuvaa jezi yenye nembo ya mdhamini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika walipocheza ugenini dhidi ya USM Alger.

Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema tayari wamefanya mawasiliano kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo.

“Baada ya kuona hitilafu zimejitokeza katika mechi ile (USM Alger vs Yanga) tulianza kuchukua hatua mapema, tukawaandikia barua TFF ambao wao ndio wanafanya direct connection na Caf kuwaeleza masikitiko yetu kwamba hatukupata fursa ya kuhudhuria mkutano wa maandalizi ambao ulikuwa unaelezea masuala yote ya udhamini na matangazo kwenye jezi.”

“Hali ile ilivyojitokeza, tukawaandikia wadhamini wetu kuwaomba radhi kwa yaliyotokea kwa sababu yalikuwa nje ya uwezo wetu. Tulilazimishwa kutotumia nembo kwa sababu ilikuwa haijasajiliwa. Tukawaandikia TFF kwamba huyu ndio mdhamini wetu mkuu hata mechi za mwanzo alikuwepo kwa hiyo tunaomba Caf wamtambue.”

“Caf wamepelekewa hiyo barua ambayo imeidhinishwa  na TFF, baada ya kufika kule wakatunibu kwamba tunaweza kutumia. Jezi zenye nembo ya mdhamini zitatumika kwa mujibu wa taratibu zao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here