Home Ligi EPL Swansea 0-Southampton 1, timu nyingine Epl yashuka daraja

Swansea 0-Southampton 1, timu nyingine Epl yashuka daraja

10757
0
SHARE

Kama ingekuwa bet baasi leo tungesema mkeka wa Mark Hughes umesoma, Manolo Gabbiadini ni kati ya washambuliaji ambao wanaonekana butu sana Southampton na tangia mwezi February tarehe 24 Manolo Gabbiadini hajawahi kufunga goli kwa Southampton katika mechi yoyote ile.

Lakini hii leo katika mchezo muhimu kabisa kwa Southampton kocha Mark Hughes alimnyanyua kwenye kiti Manolo Gabbiadini akachukue nafasi ya Jan Bednarek ili kujaribu kutafuta bao litakaloifanya Soton kubaki katika Epl msimu huu.

Dakika 4 tu baada ya Manolo kuingia alifunga bao pekee kwa Southampton katika mchezo wa leo, goli ambalo linawabakisha Southampton katika Epl na hili likiwa bao lake la 5 katika mechi 41 alizoitumikia Southampton.

Matokeo ya leo yanaifanya West Bromich kuwa timu ya pili kushuka daraja msimu huu, na hii ni mara ya 10 kwa West Bromich kushuka daraja na ni timu mbili tu ambazo zimewazidi kushuka daraja, Birmingham(12) na Leicester(11).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here