Home Ligi EPL Southampton wawekewa sumu

Southampton wawekewa sumu

7224
0
SHARE

Southmapton kwenye jaribio la mapinduzi. Mechi ya kufa na kupona ambapo itapigwa pale St Mary dhidi ya Swansea. Wikiendi hii Southampton aling’ang’aniwa na Everton kwa kutoka sare ya bado moja kwa moja ugenini. Huu nimchezo wao wa kuamua hatma yao. Safari yao ya ligi kuu imekubwa na kashakashi nyingi sana ikiwemo ukata, kuondoka ovyo kwa wachezaji muhimu pamoja na fukuza fukuza ya makocha.

Tokea Mark Hughes ajiunge na klabu hiyo imebadilika na imekuwa na mchezo wa kuvutia sana licha ya kwamba imekumbwa na gundu la kukosa matokeo sahihi. Swansea wao wamepoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Fc Bournemouth ugenini kwa bao 1-0

15 West Ham United 36 9 11 16 45 67 -22 38
16 Huddersfield Town 36 9 9 18 27 56 -29 36
17 Southampton 36 6 15 15 36 55 -19 33
18 Swansea City 36 8 9 19 27 53 -26 33
19 West Bromwich albion 37 6 13 18 31 54 -23 31
20 Stoke City 37 6 12 19 33 67 -34 30

 

Klabu ya Stoke City tayari imekwisha kushuka daraja. Hata hivyo ripota Daniel Mathews ameeleza kuwa kocha mkuu wa Southampton Mark Hughes amelalamikia uhuni uliowafanywanaa baadhi ya wahudumu wa hoteli ya Marriott kuwa kwenye vyumba vyao waliwekea sumu. Klabu ya awali ya Mark Hughes ya Stoke City imekwisha shuka daraja na sasa ana kibarua cha kuwaokoa watakatifu hawa wa soton. southampton watahitaji washinde mchezo huu ili kuongeza game la alama kati yake yeye na Swansea na West Bromwich.

Wachunguzi wa Soton walikwenda katika hotel hiyo na kugundua kula chumba kile kiwekewa virusi na hapakuwa salama kwao. Kwa sasa wanafanya mazoezi katika kiwanja Vale of Glamorgan ambacho kinatumiwa na mahasimu wakubwawa Swansea (Cardiff City).

 

Nani kuwakoa Soton

Nathan Redmond, Amekuwa na msimu mzuri hasa tokea Hughes junge nao. Amekuwa mchezaji wa muhimu sana katika kikosi chao.

Mlinda mlango wao Alex McCarthy amekuwa na kiwango bora licha ya kwamba timu yao imeruhusu magoli yaliyotibua mipango yao hasa katika michezo mitano ya mwisho. Aliokoa michomo hatario kadhaa katika michezo yao miwili dhidi ya Everton an Bournemouth. Wesley Hoedt pia atabeba jukumu la Maya Yoshida ambaye alipigwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita.

Hoedt

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here