Home World Cup Road 2 Russia: je wajua?

Road 2 Russia: je wajua?

6984
0
SHARE

Kuelekea kombe la Dunia-Russia-2018

1. Mchezaji wa kwanza kufunga goli katika michuano ya kombe la Dunia ni mchezaji wa Ufaransa Lucien Laurent dhidi ya Mexico baada ya kupokea pasi toka kwa Ernest Liberati ambapo mechi hii Ufaransa walishinda goli 4-1, mechi hii ikifanyikia katika dimba la Estadio Paesto

2. Timu ya kwanza kutwaa kombe la dunia ni Uruguay ambapo michuano hii ilifanyikia kwa mara ya kwanza Uruguay kwanzia tarehe 13 July na kumalizika tarehe 30 July 1930. Uruguay walishinda goli 4-2 Argentina magoli ya Uruguay yakifungwa na Hector Castro, Pedro Cea, Pablo Dorado na Victoriano iriarte huku magoli ya Argentina yakifungwa na Guillermo, Carlos Peucelle.. Kocha wa mabingwa hawa wa kwanza kihistoria alikuwa ni Alberto Suppicci

3. Kipa wa kwanza kuwa na clean sheet ni kipa wa USA- Jimmy Douglas.

Katika michuano hii timu nyingi kutoka barani ulaya zilishindwa kushiriki kutokana na changamoto ya kusafiri hadi barani America kusini.

4. Mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu ni mchezaji wa zamani wa Peru, Placido Galindo tarehe 14 July 1930 wakicheza dhidi ya Romania. Michuano iliyofanyikia nchini Uruguay

5. Kadi nyekundu ya mapema kabisa katika michuano ya kombe la Dunia ni ya mchezaji wa Uruguay Jose Batista katika sekunde ya 57 baada ya kumchezea mchezaji wa Scotland Gordon Strachan. Hii ikiwa ni mwaka 1986 katika michuano iliyofanyikia nchini Mexico.

6.Hawa ndo wachezaji wanaongoza kufunga magoli mengi katika michuano ya kombe la dunia.

1. Miroslave Klose
Huyu ni Mjerumani mwenye asili ya Poland anaeshikilia rekodi ya muda wote kuwa na magoli mengi akiwa na magoli 16 aliyafunga katika michuano ya mwaka 2002, 2006, 2010, 2014.

2. Ronaldo de Lima
Mchezaji hatari wa Brazil anaeshika rekodi ya pili kwa kuwa na magoli mengi akiwa na goli 15 alizofunga katika michuano ya mwaka 1998, 2002 na 2006

3. Gerd Muller
Mjerumani mwingine katika listi hii akiwa na goli 14 ambapo alifunga katika michuano ya 1970 na 1974. Rekodi hii ilidumu kwa miongo 3 kabla ya Ronaldo De Lima kuivunja.

4. Just Fontaine
Mchezaji wa Ufaransa akiwa na magoli 13 akiweka rekodi ya aina yake kwa kufunga magoli haya katika mechi 6 tuu za michuano ya mwaka 1958.

5. Edson Arantes do Nascimento “Pele”
Mchezaji wa karne ya 20 kutoka Brazil, mkongwe huyu alifunga jumla ya magoli 12, ambapo alifunga magoli haya katika michuano ya miaka ya 1958, 1962, 1966, 1970..

#Mchezaji mwenye nafasi ya kuvunja rekodi hii, kutokana na kuwa katika kumi bora ya wafungaji bora wa muda wote ni mchezaji wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich – Thomas Muller kwani ana goli 10 mpaka hivi sasa na timu yake ina nafasi ya kufika mbali kutokana na ubora walio nao na wachezaji bora katika kikosi chao,pia wakiwa mabingwa watetezi na wapo nafasi ya 1 ya timu bora duniani mpaka hivi sasa..

Imeandaliwa na Melkizedeck Mbisse.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here