Home Kimataifa Massimiliano Allegri ndiye kocha mpya Arsenal?

Massimiliano Allegri ndiye kocha mpya Arsenal?

8500
0
SHARE

Arsene Wenger ndio huyoo anaondoka Arsenal, katika wakati huu kuna maneno mengi sana kuhusu nani atakuwa mrithi wa Arsene Wenger. Kila mtu anasema lake na kila chanzo cha habari kinaandika lake.

Lakini habari ambayo ni kubwa kwa sasa ni kuhusiana na Massimiliano Allegri kocha wa Juventus, tetesi zimekuwa kubwa kwamba Allegri yuko njiani kwenda kurithi mikoba ya Arsene Wenger.

Habari kutoka Italia zinasema wamiliki wa Juventus na Allegri watakutana wikiendi hii kujadili hatma ya Allegri, kikao hiki cha Jumapili kinatarajiwa kutoa hatma ya kocha huyo katika klabu ya Juve.

Katikati ya msimu huu inasemekana Allegri aliomba kuachia nafasi katika klabu ya Juve ifikapo mwisho wa msimu huu japokuwa hakutoa taarifa rasmi lakini boss wa Juventus Giussepe Moratta anaweza kuamua hatma ya kocha huyo.

Tetesi zinasema Arsenal wanakaribia kuachana na mpango wa kumchukua Luis Enrique baada ya Enrique kutaka kiasi kikubwa cha pesa, na sasa Allegri anabaki kama namba moja katika listi ya makocha wakuchukua nafasi ya Wenger.

Kwa upande mwingine mashabiki wengi wa Arsenal wanaonekana kupinga ujio wa Allegri na kudai kwamba sio kocha type yao, Allegri ni kati ya makocha wanaopenda kukaba wakati Arsenal wao wanapenda mpira wa pasi nyingi na kushambulia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here