Home Kimataifa Lippi “Mancini anafaa zaidi kubeba mikoba ya taifa letu”

Lippi “Mancini anafaa zaidi kubeba mikoba ya taifa letu”

6415
0
SHARE

ROBERTO Mancini ameungwa mkono na aliyekuwa kocha mkuu wa Italia mwaka 2006 Marcello Lippi, achukue nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Italia.Kocha huyo wa Zenit Mancini, atafanya mazungumzo na Shirikisho la Soka Italia (FIGC) mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Urusi kwaajili ya kupata nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Italia.FIGC hapo awali ili wataja Mancini,Antonio Conte,Carlo Ancelloti na Claudio Ranieri kwenye orodha ya makocha ambao watakabidhiwa timu hiyo baada ya kushindwa kufanya vyema katika mashindano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.Lippi ambaye aliwaongoza Italia kushinda taji la Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa kocha wa timu hiyo, anaamini kwamba Mancini ni kocha mzuri na anauwezo wa kuibadilisha timu baada ya kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia.“Mancini ni kocha wa juu na ni mzoefu mkubwa wa kimataifa.”Majina yote matatu ambayo yalichaguliwa, nadhani, yamekubaliwa na mashabiki: Ancelotti, Mancini na Ranieri.,Lakini Mancini ni bora kwa upande wangu.”Ikiwa ni Mancini, hakika atakuwa kocha mwenye ujuzi mkubwa wa kimataifa, na tayari amefundisha vikosi vingi kabla, na inaonekana kuwa ana hamu kubwa ya kufundisha timu ya Italia.”alisema Lippi.====================Allegri Atakiwa Kuendelea Kubaki JuventusMASSIMILIANO Allegri ameunganishwa katika orodha ya makocha ambao wanahitajika kuchukua nafasi ya Arsene Wenger, pindi atakapo achana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.Juventus ina karibia kushinda Scudetto kwa msimu wa saba mfululizo, na ikimuacha Napoli nyuma ya pointi sita. Lakini uvumi ambao unaendelea unasema kwamba Allegri anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu.Allegri na Luis Enrique, wanatajwa kuwa makocha sahihi ambao wanaweza kuifanikisha Arsenal, ambapo wanapo ondokewa na kocha Wenger aliyedumu na klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi.Hata hivyo, mtendaji mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta, alisikika akisema kwamba bado wana nafasi kuendelea kumshawishi Allegri kuendelea kubaki na Juventus.”Sisi na Allegri tuna uhusiano mzuri baada ya kufanya naye kazi vizuri, hivyo tutatumia nafasi ya kuendelea kumbakiza hapa.”Baada ya kushinda Scudetto tutazungumza nae juu ya siku zijazo ndani ya klabu hii, ambapo nina uhakika kuwa ataridhika pamoja nasi,” alisema Marotta.Habari zote na Daniel S Fute.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here