Home Kimataifa Koscienly kulikosa kombe la Dunia

Koscienly kulikosa kombe la Dunia

6915
0
SHARE

Jeraha La Koscienly La Muweka Nje Ya Uwanja Hadi Desemba 2018

MCHEZAJI wa Arsenal Laurent Koscielny, hataweza kucheza Soka katika kipindi cha miezi sita baada ya kupata jeraha kubwa katika mchezo wa Europa League dhidi ya Atletico Madrid.

Taarifa hii imethibitishwa rasmi na kocha mkuu wa klabu hiyo Arsene Wenger, katika mazungumzo na waandishi wa habari kwaajili ya kuelekea katika mchezo wao na Leicester City hapo kesho.

Nyota huyo wa Ufaransa tayari amefanyiwa upasuaji katika jeraha lake na imethibitishwa kwamba atahitajika kupata mapumziko ya muda wa miezi sita, bila kurudi uwanjani.

Hivyo Koscielny atakuwa nje ya uwanja mpaka mnamo mwezi Desemba mwaka huu. Wenger amesikitishwa kwa mchezaji wake mwenye umri wa miaka 31, maana atapoteza miezi mitatu ya kwanza katika msimu mpya wa ligi kuu England.

Pia Shirikisho la soka la Ufaransa tayari walithibitisha kwamba, beki wao Koscielny hataweza kujumuishwa katika kikosi cha Ufaransa ambacho kitakwenda Urusi kwaajili ya Kombe la Dunia.

“Tayari yeye ameshafanyiwa upasuaji katika jeraha lake, hivyo kwa mujibu wa madaktari wamesema kwamba atahitajika awe katika mapumziko mpaka mwezi Desemba ndio arejee uwanjani,” alisema Wenger.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here