Home Dauda TV Kocha kafunguka wachezaji waliogoma kwenda Algeria

Kocha kafunguka wachezaji waliogoma kwenda Algeria

13128
0
SHARE

Wakati kikosi cha Yanga kinasafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, kuna baadhi ya wachezaji hawakusafiri na timu.

Taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa Yanga ni kwamba, wachezaji ambao hawakusafiri kwenda Algeria walikuwa na matatizo mbalimbali. Wapo waliokuwa wagonjwa, wengine walikuwa na majeraha huku baadhi ilielezwa wana matatizo ya kifamilia.

Kocha mpya wa Yanga Zahera Mwinyi amesema kuna wachezaji wakubwa wenye uzoefu watano au sita walikataa kwenda Algeria.

“Timu bado haijakutana ya wachezaji wote, kila mchezo kuna watu wanakosekana, mmeona tumeenda Algeria karibu wachezaji sita au watano walikataa kwenda.”

“Timu ipo kwenye matatizo lakini walipaswa wasubiri, wengine mikataba yao imemalizika walikataa kwenda.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here