Home Uncategorized Juventus vs Ac Milan, siku 4 za Allegri kubeba ndoo mbili kubwa...

Juventus vs Ac Milan, siku 4 za Allegri kubeba ndoo mbili kubwa zinaanza leo

8515
0
SHARE

Nchini Italia hii leo kutakuwa na mchezo mkubwa sana kati ya wababe wawili wa nchini humu Ac Milan wakimenyana na Juventus katika fainali za michuano ya Copa Italia. Endapo Juventus watashinda katika mchezo huu baasi itakuwa klabu ya kwanza Italia kushinda kombe hili mara 4 mfululizo.

Ukiacha hilo lakini pia inaonekana kama wiki nzuri sana kwa kocha Massimiliano Allegri kwani baada ya mchezo wa leo anakwenda kukutana na As Roma siku ya Jumapili katika Serie A ambapo suluhu itawapa Juve taji la 7 la Serie A, hii ina maana kuanzia leo Allegri anaweza kubeba makombe makubwa 2 nchini Italia ndani ya siku 4.

Ac Milan wenyewe mchezo wa leo wanaweza kuutumia kuondoa uhaba wa makombe uliotawala katika klabu hiyo kwani mara ya mwisho kwa Milan kubeba kombe kubwa nchini Italia ilikuwa mwaka 2011 ambapo walibeba Serie A chini ya kocha wanayekutana naye leo Massimiliano Allegri.

Juventus wana nafasi kubwa kuibuka na ushindi siku ya leo kwani rekodi yao mbele ya Milan imekuwa ikiwabeba, katika michezo minne ya mwisho kati ya timu hizi mbili Ac Milan wamepoteza mara 3 huku wakiambulia sare moja tu.

Msimu huu tu Juventus wameshawafunga Milan jumla ya mabao 5-1 na uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni ya Wachina waliochukua umiliki wa klabu hiyo inaifanya klabu ya Ac Milan, kocha pamoja na wachezaji kuwa na deni kubwa la kuonesha thamani ya kikosi chao msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here