Home Kimataifa Yanga yatoa ufafanuzi jezi kukosa nembo ya mdhamini

Yanga yatoa ufafanuzi jezi kukosa nembo ya mdhamini

7087
0
SHARE

Mkwasa

Uongozi wa Yanga kupitia Katibu Mkuu wake Charles Boniface Mkwasa umetoa ufafanuzi juu ya tukio la kutovaa jezi zenye nembo ya mdhamini katika mchezo wao wa kwanza wa kombe la shirikisho Afrika hatua ya makundi.

“Ni kweli huo usumbufu ukijitokeza na sisi tuliuona na tuliusikia lakini tulipata taarifa tangu juzi wakati wa pre match kwa hiyo hilo suala lipo na sisi kama uongozi tunalifanyia kazi.”

“Nilikuwa nafanya mawasiliano na SportPesa pamoja na TFF ili kuona tunafanyaje na baada ya hapo ofisi itatoa taarifa rasmi kuhusu nini hasa kilichotokea.”

“Tatizo lilianza siku moja kabla ya mchezo na sisi tukapata taarifa tukawa haguna namna tukapitia baadhi ya vifungu lakini ikaonekana kwamba haiwezekani.”

“Kuna utaratibu wa kushiriki haya mashindano na kanuni zake zipo lakini kwa suala ambalo limetokea jana limetufedhehesha hata SportPesa pia. Hili suala tunalifanyia kazi, tutakapokuwa tumekamilisha taratibu zote tutalitolea maelezo kama kuna mtu alizembea mahali.”

“Wasizungumze vitu ambavyo hawavifahamu wasubiri taarifa rasmi kutoka klabu halafu waendelee kujadili.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here