Home Kimataifa Yanga hakuna kulala

Yanga hakuna kulala

7651
0
SHARE

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwasili kesho ambapo moja kwa moja kitaendelea na maandalizi ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons mechi inayotarajiwa kuchezwa siku ya Alhamisi Mei 10  2018 uwanja wa Sokoine Mbeya.

Katibu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema tayari mipango ya kuisafirisha timu kwenda Mbeya imeshaanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

“Kwa mujibu wa booking yetu, timu inatarajia kuondoka Algeria alfajiri ya leo na inatarajia kufika mchana itapita njia ileile kama ilivyokwenda kwa kupitia Dubai.”

“Tuna mechi siku ya Alhamisi kwa hiyo kilichopo hapa ni mchakato wa kusafirisha timu kuipeleka Mbeya kwa ajili ya mechi dhidi ya Prisons.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here