Home Ligi EPL Warithi wa Wenger hawa hapa

Warithi wa Wenger hawa hapa

12116
0
SHARE

Massimillano Allegri

Kwa sasa yupo klabuni Juventus akipigana vikumbo na klyabu ya Napoli katika harakati za kutwaa ubingwa wua Series A. Ni kocha mwenye mafaniukio makubwa sana akiwa tayari amekwisha kutwaa vikombe 7 na Juventus, Serie A 3, na makombe mengine manne. Pia alipata mafanikio makubwa alipokuwa Serie A 1 na Supercoppa. Alianzia maisha yake kule ligi daraja la 4 katika klabu ya Aglianese kisha akatua Milan miaka 7 baadae.

Alifanikiwa kunyakua Scudetto msimu wake wa kwanza kabla mambo hapo baadae kuyumba hasa pale aliposhindwa kumzuia kiungo wao bora Andrea Pirlo kujiunga na Mahasimu wao Juventus. Amefika fainali za Uefa mbili.

Anajulikana hasa kwa mfumo wake wa kubadilisha mfumo asilia wa mabeki na kutumia zaidi mabeki watatu. Mfumo wake hasa ni kumiliki mpira na kukaba kwa nguvu kitu ambacho kitawavutia zaidi mabosi wa The Gunners.

Carlo Ancelotti

Baada ya kutimuliwa klabu Bayern Munichen msimu huu pia alaitajwa sana kunyakua mikoba ya Arsen Wenger. Katika miaka yake 8 ya Milan alinyakuwa Serie A moja, uefa mbili na alifika fainali ha uefa moja ambayo alipoteza kwa Liverpool.

Ni kocha mkubwa na mwenye heshima ya kipekee. Uefa imekuwa ndoto za mchana kwa wana gunners. Ancelotti tayari ni kocha ambaye ana uzoefu mkubwa wa kombe hivyo ataleta motisha zaidi. 2009 alijiunga na Chelsea ambapo alinyakua Makombe mawili (EPL na FA). Alipotua Madrid aliwapa kombe la 10 la uefa kabla hajafukuzwa. Ni kocha mbabe na mwenye maamuzi ya kipekee. Ni injinia mzuri wa soka.

Diego Simeon

Licha ya kwamba aliongeza mkataba hadi 2020 lakini bado nae anatajwa sana kujiunga pale Emirate Stadium. Wenger ni kocha ambaye aliwekeza zaidi kwenye mfumo wa kumiliki mpira zaidi kuliko adui yako.

Kwa Simeoni ni tofauti kabisa. Simeoni yeye anaamini kwanza kwenye vita cha muhimu kujiuzuia kwanza . anajali zaidi uhai wake kuliko kifo cha adui yake. Simeon amekuwa mpambana mwemye umbile dogo lakini uwezo wake ni mkubwa kushindana na wapinzani wake wenye miili mikubwa.

Kwa zaidi ya miaka 10 ameweka rekodi ya kupambana na Barcelona na Madrid na hii ni moja ua historia kubwa ndani ya la liga. Amefika fainali za uefa mara mbili na amekwisha kubeba laliga mara moja.

Joachim Low

Anataka kujaribu nae nafasi yake kwenye vilabu kwa mara nyingine tena. Aliwahi kufanya kazi VfB Stuttgart ambapo alitwa kombe la DFB pokal mwaka 1996. Hii ni riski kubwa sana kwake na kwa arsenal pia.

Ametimiza miaka 58 mwaka huu mwezi wa pili. Kocha bora wa dunia mwaka 2014. Alitwaa kibarua cha kuinoa ujerumani mwaka 2006 alipokuwa kocha msaidizi chini ya Jurgen Klinsmann. Katika mashindano makubwa matano amepoteza nusu fainali mara 3(2010, 2012, 2016) na fainali moja ya Euro 2008 na kutwa kombe la dunia. Shukrani kwa Mario Gotze. Uzoefu na utashi wake huenda ukampa mikoba ya Wenger. Je atafanikiwa mimi sijui

Thomas Tuchel

Sio jina kubwa sana. Hana mafanikio makubwa kivile. Lakini kutokana na ufundishaji wake ametajwa sana kwenda london. Ana miaka 41. Bado ni mdogo sana.

Ni kocha wa malengo na mipango ya muda mrefu kama ukimpata. Alipokea mikoba ya Jurgen Klopp aliyeonekana kusuasua sana msimu wake wa mwisho. Alibadili mfumo mzima wa timu. Baadhi ya wachezaji walionesha makali yao akiwemo Aubemayang. Chini ya utawala wake BVB walimaliza wa pili msimu wake wa kwanza. Licha ya kutwaa ubingwa wa DfB Pokal siku tatu baadae alitimuliwa mwaka 2017.

Alianzia kibarua chake pale Ausburg 2007. Kisha akatimkia Mainz ambayo aliitoa nafasi ya 9 mpaka ya 5. Anapenda vijana wadogo, ni mwalimu mzuri. Kiufupi ni fundi. Shida hana mtaji. Je Akina Kreonke watamwamini? Mimi sijui.

Patrick Viera

Mchezaji wa zamani wa Arsenal huyu nae ametajwa kwenye orodha hii. Huyu ndiye nahodha wa mwisho wa Arsenal kunyanyua kwapa la kubeba kikombe la ligi kuu England mwaka 2004. Alistaafu soka 2011. Aliingia kwenye benchi la ufundi na maendeleo la Man City kwa miaka miwili kisha 2015 alikwenda kuifundisha New York City ya marekani.

Uzuri wake anaijua Arsenal vizuri, na ni moja ya watu wenye motisha mkubwa vyumba vya kubadilishia nguo. Konda ametaka usukani kazi kwa mmiliki wa basi. Hapo hapo pia Thiery Henry nae ametajwa kutwaa mikoba hiyo.

Wengine waliotajwa ni Eddie Howe kocha wa FC Bournemouth mwenye umri wa miaka 40. Hata hivyo David Seaman ameishauri bodi ya Arsenal kupata kocha mwenye uzoefu mkubwa. Brendan Rogders Kocha wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Celtic ne pia ametajwa kuwania viatu vya Wenger

Imeandaliwa na Privaldinho (Instagramm)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here