Home Kimataifa Tuliyoyaona wikiendi hii kule majuu

Tuliyoyaona wikiendi hii kule majuu

11993
0
SHARE

Na Melkizedeck Mbisse

1. Cristiano Ronaldo baada ya kufunga goli 1 katika sare ya 2- 2 dhidi ya Barcelona, Ronaldo ameifikia rekodi iliyokuwa inashikiliwa na gwiji wa Real Madrid, Alfredo Di Stefano ya mchezaji wa Real Madrid mwenye magoli mengi katika pambano la watani wa jadi al maarufu kama El Clasico, wote kwa sasa wakiwa na magoli 18.

2. Kiungo wa Manchester City na Mbeligiji, Kevin De Bruyne amefikisha jumla ya mechi 100 za ligi kuu Uingereza akichezea timu yake dhidi ya Huddersfield walipoenda sare ya bila kufungana. Katika mechi hizo De Bruyne ana jumla ya magoli 21 na pasi za mabao/assists 43.

3. Kiungo wa SSC Napoli, Mslovakia Marek Hamsik, amefikisha jumla ya magoli 100 katika ligi kuu ya Italy -Serie A akiwa na SSC Napoli, ambapo alifunga goli 1 katika droo ya 2-2 ya timu yake Napoli dhidi ya Torino.

4. Baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kufunga goli 1 kila mmoja katika El Clasico, wote kwa pamoja wamefunga jumla ya magoli 1000 katika vilabu vyao. Lionel Messi amefunga jumla ya magoli 551 na Cristiano Ronaldo amefunga jumla ya magoli 449 hivyo ukijumlisha wote kwa pamoja unapata jumla ya magoli 1000.

5. Baada ya kiungo mahiri wa Barcelona, Andres Iniesta kucheza El Clasico yake ya mwisho, zifuatazo ni takwimu ya mechi za El Clasico alizoshiriki. Amecheza jumla ya mechi 38, ameshinda 16, amedroo mechi 10 na kupoteza mechi 12.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here