Home Kimataifa “Nilipokiona kikosi cha Yanga niliamua kulala”-Tiboroha

“Nilipokiona kikosi cha Yanga niliamua kulala”-Tiboroha

12539
0
SHARE

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema baada ya kuona kikosi cha Yanga kilichopangwa kucheza dhidi ya USM Alger aliamua kupiga chini kufuatilia mechi hiyo badala yake akalala.

Dkt. Tiboroha hakuufuatilia mchezo huo kwa sababu hakuona kama kuna mpango wa kupata matokeo kulingana na kikosi kilichosafiri kutoka Dar kwenda Algeria

“Nilipoangalia kikosi niliondoka kwenda kulala kwa sababu nilijua kwa wachezaji waliopangwa na kikosi kilichoondoka Tanzania hatukuwa na mipango yoyote ya kupata matokeo.”

“Kama mwalimu unajua unakwenda kucheza na timu gani unatakiwa kucheza ‘pre cautionary game’ na hiyo unatakiea kuicheza kuanzia kwenye lineup. Tulipanga lineup utafikiri tunaenda kucheza na Ihefu ya Mbeya.”

“Kitu ambacho kinanipa wasiwasi ni juu ya benchi letu la ufundi kama linauelewa wa mashindano tunayoshiriki ni mashindano ya aina gani.”

“Huwa nawaambia watu ligi ya Tanzania sio kipimo cha mashindano na ninayo mifano mingi ya kuonesha. Jiulize kwa nini unapokuwa bingwa wa Tanzania unafungwa 4-0 na bingwa wa nchi nyingine au unapokuwa bingwa wa Tanzania unasumbuliwa na ‘vitimu vingine’ vidogovidogo vya Kusini mwa Afrika.”

Dkt. Tiboroha ameishauri pia Yanga nini cha kufanya katika mashindano hayo ya pili kwa ukubwa  Afrika kwa ngazi za vilabu.

“Ubingwa Tanzania sio kipimo kabisa katika mashindano ya Afrika, mashindano ya Afrika ni kitu kingine, ni mashindano makubwa yanayokutanisha vilabu vikubwa ambavyo vipo serious vilivuoendelea nje na ndani ya uwanja.”

“Inatakiwa unapokwenda katika mashindano hayo uwe umejipanga kimbinu na kimikakati. Ni vitu ambavyo napoviangalia kama mdau wa mpira nashindwa kuelewa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here