Home Kimataifa Haji Manara baada ya Yanga kufungwa 4-0 kimataifa

Haji Manara baada ya Yanga kufungwa 4-0 kimataifa

9821
0
SHARE

Baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa kombe la shirikisho Afrika hatua ya makundi kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya USM Alger, Haji Manara Yanga wanaidhalilisha Tanzania nje ya nchi.

Manara amesema licha ya Simba kutupwa nje ya mashindano hayo mapema, lakini ilitoka kwa heshima tofauti na watani zao na kuongeza kuwa huu ni msimu wa mwisho kwa Yanga kupanda ndege.

“Nimesikitika sana, nimejisikia vibaya kama mtanzania nahisi kuna watu wanatumiwa na mabeberu wanyonyaji kuihujumu nchi kwa sababu tumepata fedheha kama taifa hilo ndio linasikitisha.”

“Najisikia mnyonge sana bendera ya nchi inadhalilishwa ugenini kila mara na nimeliomba Bunge likae kama kamati kama wataweza wajadili hili jambo kwa sababu nchi inafedheheshwa sana ugenini.”

“Tunachoshukuru wanamaliza ndege yao ya mwisho kutoka Algeria, wakirudi najua watatambaa kuelekea Kigali na Nairobi na mwakani watakuwa hapahapa wanacheza ligi ya nyumbani wakisafiri watakuwa wameenda kucheza Mapinduzi Cup.”

“Sisi tumecheza mechi zetu hatukufungwa hata mechi moja, Waarabu waliomba mpira uishe kwao. Tulitolewa kwa heshima, hatuzungumzii kutokufungwa tunazungumzia kufungwa kwa dharau. Leo hadi spika wa Bunge kasimama unadhani jambo dogo?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here