Home Kitaifa “TFF wamecheza vizuri mechi ya nyumbani bado ugenini”-Michael Wambura

“TFF wamecheza vizuri mechi ya nyumbani bado ugenini”-Michael Wambura

9067
0
SHARE

Aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura anatarajia kuchukua hatua nyingine mbele kupinga adhabu yake ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi chote cha maisha yake.

Wambura akiwa kwenye kipini cha Clouds 360 siku ya Jumamosi Mei 5, 2018 alisema wanasheria wake wameshafikia uamuzi na kilihobaki ni utekelezaji.

Amesema TFF wamecheza vizuri mechi yao ya nyumbani kwa maamuzi waliyofanya kilichobaki sasa ni kucheza ugenini.

“Huwezi kuwa bingwa kwa kucheza nyumbani, ukitaka kuwa bingwa mzuri lazima ucheze na away. Ninachoamini TFF wamecheza uwanja wa nyumbani, wameutumia uwanja wao wa nyumbani vizuri kwa maamuzi waliyoyafanya.”

“Bado kwenda kucheza uwanja mwingine, tutakwenda kucheza uwanja mwingine na matokeo yanaweza kupinduka kama Barcelona na AS Roma.”

“Kushindwa kufanikiwa kwa jambo la mwanadamu ni siku anapokuwa amekufa, nitaendelea mbele popote ambapo mwanasheria wangu ataona inafaa kwa sababu kwa mujibu wa sheria kwa sasa mimj sio mwanafamilia wa mpira.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here