Home Kitaifa “Soka la Tanzania linahitaji jembe la ng’ombe”-Michael Wambura

“Soka la Tanzania linahitaji jembe la ng’ombe”-Michael Wambura

9001
0
SHARE

Kwa nama soka la Tanzania linavyokabiliwa na changamoto mbalimbali, unaambiwa dawa ya hayo yote ni kufanya mageuzi  kama sio mapinduzi yani ‘juu chini, chini juu’ kama ambavyo jembe la ng’ombe linavyolima.

Maneno hayo sio yangu ni ya aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura wakati akizungumza kwenye kipindi cha Clouds 360 ndani ya Clouds TV Jumamosi Mei 5, 2018.

Wambura amesema kwa aina ya mfumo uliopo sasa haoni kama soka la Bongo linaweza kupiga hatua kwa sababu kuna kikundi cha watu wachache wanadhani mchezo wa soka ni mali yao.

“Soka la Tanzania linahitaji jembe kama linalokokotwa na ng’ombe, likipita ugongo wa chini unakuja juu wa juu unakwenda chini. Mfumo tulionao sasa sioni kama tunaweza kupiga hatua kawa sababu kikundi cha watu wachache ambao wanadhani mchezo wa mpira wa miguu ni mali yao.”

“Mfumo wa Fifa ulivyo hauruhusu watu kutoka nje kuingia ndani kirahisi, kinachoendelea sasa hivi ni kutengeneza mfumo wa kuwafanya watu fulani wabaki wao na wewe kutoka nje hutopata nafasi ya kuingia.”

“Kwa mfano kama mimi nateua kamati ya uchaguzi na kamati ya rufaa unapofika wakati wa uchaguzi mtu ambaye hawamtaki ataambiwa hajakidhi vigezo.”

“Lazima tutoe nafasi kwa watu wenye nia njema na vigezo wakagombea badala ya kuwaondoa na kuwaweka wanaowataka wao.”

“Kuna watu wengine wanaogopa kuingia kwenye mpira na kugombea nafasi za uongozi kwa sababu wanaona kuna uhuni na wanaogopa kudhalilishwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here