Home Kitaifa Okwi kazungumzia rekodi inayoshikiliwa na Tambwe

Okwi kazungumzia rekodi inayoshikiliwa na Tambwe

13905
0
SHARE

Okwi anaongoza katika orodha ya wafungaji wa VPL hadi sasa akiwa amefunga magoli 20, anahitaji magoli mawili ili avunje rekodi ya Amis Tambe aliyoiweka msimu wa 2015/16 ambapo alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga magoli 21.

Okwi anahitaji goli moja kufikia rekodi ya Tambwe (magoli 21) ambayo ni magoli mengi zaidi katika kipindi cha misimu 10 iliyopita, akifunga magoli mawili atakuwa ameivunja rekodi hiyo.

Baada ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Ndanda, Okwi amesema rekodi hazimpi presha anachoangalia zaidi ni timu yake kupata pointi tatu.

“Rekodi za watu haziwezi kunipa presha, ninachoangalia ni kuisaidia timu yangu kupata pointi tatu, ninapofanikiwa kufunga ni vizuri zaidi”-Emanuel Okwi, mshambuliaji wa Simba.

Kwa mechi za karibuni Simba imekuwa ikipata ushindi wa magoli machache ukilinganisha na siku za nyuma, Okwi amesema wakati mwingine sio lazima yeye na Bocco kufunga bali muhimu ni timu kupata matokeo.

“Inatokana na ushindani kwa sababu huwezi kufunga kila siku, wakati mwingine mabeki wa timu pinzani wanakaza kwa hiyo muhimu kwetu ni timu kushinda na kupata pointi tatu sio mimi na Bocco kufunga ndio maana mechi iliyopita (Simba vs Yanga) alifunga Erasto Nyoni.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here