Home Kitaifa Ngasa baada ya game Simba vs Ndanda

Ngasa baada ya game Simba vs Ndanda

11504
0
SHARE

Mrisho Ngasa bado anaamini Ndanda FC itafanikiwa kubaki ligi kuu licha ya kupoteza mhezo wao dhidi ya Simba kwa kufungwa 1-0 huku wakiwa wamebakiza mechi tatu kabla ya ligi kumalizika.

Ngasa amesema wanahitaji kucheza kwa hesabu mechi zao tatu zilizobaki ili kuhakikisha wanasalia VPL.

“Nafasi yetu ni ngumu tunatakiwa kucheza kwa hesabu sana kwa sababu tumebakiza mechi tatu halafu Majimaji imetoka sare na Mtibwa kwa hiyo wanatuzidi pointi moja.”

“Tuna michezo miwili nyumbani mmoja ugenini, nafasi bado ipo kwa sababu tulikuja hapa kutafita draw lakini imeshindikana kwa sababu Simba wametumia nafasi moja walioipata wamepata matokeo.”

“Kucheza katika timu ndogo ni tofauti na timu kubwa kwa sababu kwenye timu ndogo kuna wakati mnatengeneza nafasi lakini mtu anashindwa kumalizia.”

Ndanda ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 27, kuanzia nafasi ya 11 ambayo ipo Mbeya City haipo salama hadi nafasi ya 16 ambako ipo Njombe Mji. Msimu huu timu mbili za chini zitashuka kwenda kucheza ligi daraja la kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here