Home Kitaifa Majibu ya Michael Wambura ukimwambia aachane na soka

Majibu ya Michael Wambura ukimwambia aachane na soka

11600
0
SHARE

Kama unakumbuka vizuri aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura alifungiwa maisha kujihusisha na soka, maamuzi ambayo yalitangazwa na kamati ya maadili ya TFF baada ya kujiridhisha na tuhuma ambazo zilikuwa zikimkabili Wambura.

Baadaye Wambura alikata rufaa kwenda kamati ya maadili ya rufaa ambako maamuzi yalibaki vilevile, inawezekana wadau wengi wanatamani kujua Wambura atachukua hatua gani au amekubali kutumikia hukumu yake?

Jumamosi ya Mei 5, 2018 Wambura akiwa ndani ya kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV ametoa msimamo wake juu ya hukumu iliyotolewa na kamati ya rufaa ya maadili na hatua atakazochukua.

“Kuna mtu akila vijiko viwili vya wali anashiba, kuna mwingine akila kilo moja ya ugali hashibi. Kama mtanzania nina wajibu wangu na bahati nzuri sisi wakati tunakua tulitunzwa, tumelelewa na kusomeshwa na serikali, kuacha ile elimu niliyosomeshwa na serikali ikapotea bure bila kuwasaidia wengine nadhani ni dhambi ambayo sistahili kuibeba.”

“Sisemi kwamba lazima niwe kiongozi, lakini mchango wangu kwenye mpira si dhani kama utakuwa umeishia hapo. Tangu 2004 sikuwahi kuwa kiongozi lakini mchango wangu katika mpira umeleta mambo mengi.”

“Nikisema niachane na mpira je, wale watu walionichagua wapo tayari kuachana na mimi?  Kuna aina mbili za watu, kuna watu ambao wanatamani uongozi lakini hawachaguliki. Ukimpeleka kwa wananchi wapigie kura hawamchagui, mimi nikipelekwa kwenye kura nachagulika, maana yake watu wanaopiga kurawananiamini.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here