Home Kimataifa Madrid walazimishwa suluhu na Barcelona waliokuwa pungufu

Madrid walazimishwa suluhu na Barcelona waliokuwa pungufu

11175
0
SHARE

Ilikuwa siku nzuri sana hii leo pale Escape One, baada ya kumuona Giroud akiiua Liverpool usiku huu tulimalizia kwa kuiona El Clasico ambapo wababe wawili wa Hispania walitoka wakigawana alama.

Alianza Luis Suarez kuipatia Barcelona bao la kuongoza, na hili linakuwa bao la 30 kwa Luis Suarez katika michezo 48 ambayo ameitumikia Barcelona kwa msimu huu tu.

Cristiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid bao hilo na hili likiwa bao la 18 kwa Mreno huyo. Kwa idadi hiyo ya mabao sasa Ronaldo anakuwa amemfikia mchezaji wa zamani wa Madrid Alfredo Di Stefano kwenye mabao ya Clasico, na hili likiwa bao lake la 449.

Sergi Roberto alipewa kadi nyekundu na ikiwa ni kadi ya kwanza ya Barca wanapewa katika Nou Camp katika michezo ya El Clasico 50 iliyopita. Pamoja na kuwa pungufu lakini Barcelona walipata bao la pili kupitia Lionel Messi.

Lakini katika kitu cha ajabu ni kwamba hili ni bao lake la kwanzaMessi la El Clasico Nou Camp tangu mwaka 2012, mabao yake 7 yaliyopita katika El Clasico kabla ya hii leo aliyafunga ugenini.

Gareth Bale aliisawazishia Real Madrid na matokeo kuisha kwa mbili mbili, hili ni bao la kwanza la Bale El Clasico na Barca ndio timu ambayo Bale amecheza mechi nyingi dhidi yao bila kufunga(8), timu nyingine ni Atletico Madrid na Everton(8).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here