Home Kimataifa Jurgen Klopp hajawahi kufungwa na Chelsea katika EPL, Conte anavunja rekodi hii...

Jurgen Klopp hajawahi kufungwa na Chelsea katika EPL, Conte anavunja rekodi hii leo? Twenzetuni Escape One

9359
0
SHARE

Liverpool wamekwenda fainali ya michuano ya Champions League na wako katika kiwango kizuri sana kwa sasa, lakini hii leo watakuwa majaribuni tena pale watakapoitembelea Chelsea pale Stamford Bridge, utamu wa mchezo huu ni mahala tunapouangalia. Wote tunakwenda Escape One kuuona mchezo huu live kwenye screen kubwa pembeni ya bahari.

Katika michezo sita iliyopita baina ya miamba hii miwili, Liverpool hawajawahi kupoteza mchezo hata mmoja na katika mechi hizi kuna michezo miwili ambayo Liverpool walishinda wakiwa ugenini.

Lakini kuna michezo 13 mfululizo ambayo Liverpool wamecheza na Chelsea na yote waliruhusu nyavu zao kuguswa(hawakuwa na clean sheet) na hii ndip idadi ndefu ya Liverpool kucheza mechi mfululizo na kuruhusu wavu wao kuguswa tangu iwatokee hivyo mwaka 1947 vs Blackburn.

Chelsea nao wanaonekana wako vizuri kwa kipindi hichi, michezo yao minne iliyopita katika mashindano yote walishinda lakini wameambulia alama moja tu katika michezo yao miwili iliyopita ya nyumbani.

Lakini rekodi ya Chelsea dhidi ya timu ambazo zipo sita bora msimu huu sio nzuri, katika michezo yao tisa dhidi ya timu hizo. Chelsea wamefanikiwa kushinda michezo miwili tu.

Wakati Olivier Giroud  akiwa amefunga mabao 4 katika mechi zake nne alizoanzishwa dhidi ya Liverpool, Mo Salah naye amefunga katika mechi zote nne za mwisho alizokutana na Chelsea akiwa Basel na Liverpool.

Rekodi zinaonesha kocha wa Liverpool Jurgen Klopp hajawahi kupoteza mchezo wowote mbele ya Chelsea katika michuano ya EPL, hadi sasa amekutana nao mara 5 akawafunga mara 2 na kutoka suluhu 3.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here