Home Kitaifa Imebaki pointi moja Simba kutangaza ubingwa

Imebaki pointi moja Simba kutangaza ubingwa

12087
0
SHARE

Imebaki pointi moja tu iki Simba itangazwe bingwa mpya wa VPL 2017/18 wakiivua Yanga taji hilo ambalo wamelichukua misimu mitatu mfululizo iliyopita.

Simba imefikisha jumla ya pointi 65 baada ya kucheza mechi 27, kimahesabu Yanga pekee ndio timu ambayo bado ipo kwenye mbio za ubingwa ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza michezo 24 ya ligi kuu.

Endapo Simba itapata pointi moja au tatu kwenye mchezo wake wa ugenini Mei 13, 2018 dhidi ya Singida United, moja kwa moja itafikisha pointi 66 (ikitoka sare) au 68 (ikishinda) hivyo kuwa mabingwa wa msimu huu.

Yanga ikishinda mechi zake zote sita (6) za VPL zilizobaki itafikisha pointi 66 ambazo endapo Simba inaweza kufikisha ikitoka sare dhidi ya Singida United lakini Simba ina wastani mzuri wa magoli kuliko Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here