Home Kitaifa “Andaeni sare za ubingwa”-Kapombe

“Andaeni sare za ubingwa”-Kapombe

10204
0
SHARE

Baada ya Simba kushinda 1-0 game ya leo dhidi ya Ndanda, ‘Wekundu wa Msimbazi’ wamezidi kuusogelea ubingwa wa VPL wakihitaji pointi moja tu kutangaza ubingwa.

Shomari Kapombe amewaambia mashabiki wa Simba waanze kuanda sare kwa ajili ya kusherekea ubingwa msimu huu.

“Dhamira yetu ni kuchukua ubingwa wa VPL, hadi sasa tuna asilimia 99.5 ya kuwa mabingwa, mashabiki wa Simba wendelee kushona sare za kusherekea ubingwa”-Shomari Kapombe.

“Tunaenda kucheza mechi na Singida United mashabiki wa Simba waje kwa wingi kushangilia ubingwa wao.”

Kapombe alikuwa nje ya kikosi cha Simba kwa zaidi ya miezi sita akiuguza majeraha aliyoyapata wakati anaitumikia timu ya taifa, ameeleza kinachomfanya kuwa katika ubora alionao sasa licha ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Kujituma jambo jingine nawashukuru walimu wangu kwa kunipa sapoti na nafasi ya kuonesha nilichonacho lakini nawashukuru pia wachezaji wenzangu kwa kunipa sapoti nilipokuwa mgonjwa na niliporudi walinipa ushirikiano ili kufikia malengo yangu.”

Simba imebakiza mechi tatu huku ikiwa na pointi 65, ikipata pointi moja itafikisha pointi 66 ambazo Yanga watazigikia kama watashinda mechi zao zote sita zilizobaki. Hata kama Yanga watafikisha pointi 66 bado Simba ina wastani mzuri wa magoli zaidi ya wapinzani wao endapo ubingwa itabidi uamuliwe kwa wastani wa magoli.

Ikibidi ubingwa kuamuliwa kwa mechi zilizowakutanisha msimu huu ‘head to head’ Simba bado itashinda ubingwa kwa sababu ilitoka sare katika mchezo wa kwanza na kushinda mechi ya mzunguko wa pili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here