Home Kimataifa Wachezaji 10 katika El Clasico wanaolipwa zaidi

Wachezaji 10 katika El Clasico wanaolipwa zaidi

11787
0
SHARE

Jumapili hii hapa moto utawaka nchini Hispania wakati Barcelona wakiikaribisha Real Madrid, kuna takwimu na mambo mengi kuhusu mchezo huu lakini hawa ndio wachezaji 10 ambao wanalipwa pesa nyingi na watakuwepo katika mchezo huo.

10.Sergio Busquets. Nafasi ya 10 inashikiliwa na kiungo kitasa wa Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Hispania, Serio Busquets kila wiki anaingiza kiasi cha £180,000.

9.Toni Kroos. Wakati nafasi ya 10 ni kiungo wa Barcelona, nafasi ya 9 pia inakwenda kwa kiungo lakini huyu ni kiungo wa Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos anayeingiza £200,000 kwa wiki.

8.Osmane Dembele. Pamoja na majeraha ambayo yamekuwa yakimuandama kinda huyu wa Kifaransa tangu anunuliwe na Barcelona akitokea PSG lakini haimzuii kuingiza kiasi cha £200,000 kila wiki.

7.Marcelo. Beki wa kushoto wa Kibrazil ambaye kwa sasa ni kati ya beki namba 3 bora kabisa ulimwenguni naye yuko katika orodha hii akikunja kiasi cha £200,000 kila wiki.

6.Sergio Ramos. Moja ya roho ya Real Madrid, pamoja na uwezo wake mkubwa katika kukaba lakini Ramos ni kama shabiki wa Real Madrid kwa namna anavyojitoa katika klabu hii inayompa £200,000 kila wiki.

5.Phillippe Coutinho. Usajili wake kutoka Liverpool kwenda Barcelona ulikuwa gumzo sana, na Barca walitumia nguvu kubwa ya pesa na ukubwa wao kumshawishi Coutinho, wanamlipa £240,000 kwa wiki.

4.Luis Suarez. Kama ilivyo kwa Coutinho, huyu naye alinunuliwa kutoka Liverpool na tangu ajiunge Barcelona amekuwa mchezaji muhimu mno, analipwa £260,000 kila wiki.

3.Gareth Bale. Bale amekuwa mchezaji ambaye anatumia muda mwingi nje ya uwanja kutokana na majeruhi, lakini hii haimzuii kuwa namba 3 katika wachezaji wanaolipwa sana El Clasico akikunja £350,000 kila wiki.

2.Cristiano Ronaldo. Moja kati ya masuala matamu ya El Clasico ni kwamba achilia mbali uwepo wa wachezaji wawili bora duniani bali pia kuna wachezaji wawili wanaolipwa zaidi Ulaya, Cristiano Ronaldo analipwa £365,000 kila wiki.

1.Lionel Messi. Mshambuliaji nyota wa Argentina yuko katika kilele cha wachezaji wanaolipwa zaidi katika El Clasico, Messi analipwa £500,000 kila mwisho wa wiki.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here