Home Kimataifa Tumuombeeni Sir Alex Ferguson, ameshafanyiwa upasuaji

Tumuombeeni Sir Alex Ferguson, ameshafanyiwa upasuaji

9611
0
SHARE

Jioni hii kumeibuka habari kwamba kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson hali yake kiafya sio nzuri kiasi cha kukimbizwa hospitali na kila mtu kuanza kusema lake.

Lakini taarifa rasmi kutoka katika klabu ya Manchester United inasema SAF amefanyiwa upasuaji hii leo, upasuaji wa SAF unahusisha ubongo na upasuaji huo umeenda vizuri japo bado SAF atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Mtoto wa Sir Alex aitwaye Darren Ferguson ambaye ni kocha wa klabu ya Doncaster alishindwa kuhudhuria mechi ya klabu ya dhidi ya Wigan baada ya kukimbilia Hospitali kufuatilia hali ya mzazi wake.

Majirani wa eneo analoishi Sir Ferguson maeno ya Cheshire nchini Uingereza wamedai kwamba hii leo wakati wa Break Fast kulikuja Ambulance ya dharula ambayo ilimbeba kocha huyo na kumkimbiza Hospitali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here